Kocha
wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
kushoto akimkabidhi sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya
shughulizake Deer Park, Victoria,
Australia mtoto
Mohamed Mussa wa Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia
namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka
wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto
akitoa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia kwa mtoto Kauthar Seif wa Madrasatul Nool Hudaa iliyopo mtaa wa mafia Dar es Salaam Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka
wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akigawa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia kwa watoto wa
Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri
ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria,
Australia
amewakumbuka ndugu zake kwa kutoa sadaka kwa watoto wa Madrasatul _Noor-Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33
akizungumza baada ya kutoa msaada uho kwa niaba ya Kimweri Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mfano uhu ni wakuigwa kwa mabondia mbalimbali
kukumbuka kutoa sadaka japo kidogo kwa kipato wanachokipata kupitia mchezo wa masumbwi
aliongeza kwa kusema kuna mabondia wengi nchini wanapata pesa nyingi kupitia mchezo wa ngumi lakini awawakumbuki watu wenye mahitaji mbalimbali
Kimweri anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title
utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri mpaka sasa amepanda
uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa
ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
bondia huyo mtanzania anaefanya
shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya
mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
na akishinda mchezo uho
itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa
wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na
mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii
ya feb 26
Kimweri alitoa shukrani za
kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka
sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni
Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli ,
Rajabu Mhamila 'Super D'
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
ambao amekuwa chachu katika
mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama
anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake
ndipo kilipozikiwa
No comments:
Post a Comment