Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi mama mzazi wa marehemu Mohamed
Chibumbui Hadija Likamba ubani uliotolewa na wadau mbalimbali wa
mchezo wa masumbwi nchini kutoka Tanzania Boxing Fans pamoja na chama
cha ngumi za ridhaa BFT katikati ni Baba mzazi Said Chibumbui Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta
Rwakatare katikati akimkabidhi Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi
Rajabu Mhamila 'Super D' mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa
ajili ya lambilambi ya marehemu Mohamed
Chibumbui kilichotokea
Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Masasi kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho
hilo Makole Mashaga Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekabidhi fedha za lambilambi kwa wafiwa wa bondia Mohamed
Chibumbui ambaye alikuwa anachezea timu ya taifa ya mchezo wa masumbwi nchini
Chibumbui aliefaliki feb 10 alikuwa anasumbuliwa na ugojwa wa kisukari na alizikwa feb 13 katika kijiji cha Mihima kata ya Namupa Tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi
Bondia Mohamed Chibumbui aliezaliwa April 24 mwaka 1988
Alianza kujifundisha mchezo wa masumbwi mwaka 2003 akiwa chini ya kocha Juma Urungu 'Mkebezi' na timu ya mavituzi
baada ya hapo aliamia timu ya polisi kisha timu ya JKT na mwisho mapaka kifo kinamkuta alikuwa akichezea timu ya Magereza
akizngumza wakati wa kupokea ubani uho uliotolewa na wadau mbalimbali wa masumbwi wakiongozwa na
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT na Tanzania Boxing Fans 'TBF' inayowakutanisha wadau mbalimbali kwa njia ya mtandao wa Watsap Group mama wa marehemu
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT na Tanzania Boxing Fans 'TBF' inayowakutanisha wadau mbalimbali kwa njia ya mtandao wa Watsap Group mama wa marehemu
Hadija Likamba ameshukuru kwa kufikiwa na lambilambi hiyo kutoka kwa wadau wa mchezo wa ngumi nchini na kuzidi kuwaombea duwa ili mchezo wa ngumi usonge mbele
Nae baba wa marehemu Said Chibumbui amewashukuru wadau wote na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega ambapo watakaa kikao kwa ajili ya alobaini ya marehemu na kufikishiwa taharifa
Marehemu alimuowa Ratifa Adrea june 7 mwaka 2008 na kubahatika kupata watoto wawili mmoja ni Alhaj Mohamed Chibumbui (7) na Abubakari Mohamed Chibumbui (2) jumla marehemu ameacha watoto wawili na mke mmoja
aliongeza kwa kusema kuwa shughuli nzima ya alobaini itafanyika nyumbani alipozaliwa marehemu tndika azimio tambukareli eneo la maputo
No comments:
Post a Comment