Bondia Shabani Kaoneka akipima uzito kwa ajili ya mp[ambano wake kesho
NA MWANDISHI wetu
MABONDI fransic Cheka na Geard Ajetovic wamepima uzito kwa ajili ya pambano lao la mabara la uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF) ambapo waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, atawaongoza Watanzania kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, kushuhudia pambano la ubingwa wa Mabara wa WBF Intercontinental kati ya Francis Cheka na Geard Ajetovic. Cheka anamkaribisha Ajetovic, Mwingereza mwenye asili ya Serbia, katika pambano hilo la raundi 12 uzito wa Super Middle, linalotazamwa kama marudiano ya mtifuano baina ya wawili hao waliowahi kuchapana jijini Manchester, Uingereza mwaka 2008. na Cheka kupoteza mpambano uho kwa point Wawili hao wametambiana vya kutosha, kila mmoja akijinasibu kuwa yu tayari kumuadabisha mwenzake, Cheka akienda mbali zaidi kwa kusema hatarajii kuwaangusha Watanzania, hususani anapopigana katika ardhi ya nyumbani. Pambano hilo limeratibiwa na Kampuni za Advance Security kwa kushirikiana na Hall of Fame Boxing and Promotions zote za Dar es Salaam, ambalo litatanguliwa na mapambano mengine manne, ikiwamo burudani ya muziki kutoka kwa Bendi ya Twanga Pepeta. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa upimaji uzito, Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile, alisema maandalizi yote ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumsapoti Cheka. Ndambile, alisema viingilio vimegawanyika makundi mawili, ambako kiingilio cha juu kitakuwa ni Sh. 50,000 kwa Jukwaa la VIP, wakati cha chini ni Sh. 15,000 kwa viti vya kawaida. Aliyataja mapambano ya utangulizi kuwa kati ya Mohammed Matumla dhidi ya Mustapha Dotto (uzito wa Light raundi nane), Mohammed Bakari na Cosmas Cheka (Feather raundi nane) na lile la Lulu Kayage dhidi ya Mwanne Haji (Fly Raundi sita)a ajili ya
mpambano wake
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo
vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na
kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment