Tangazo

Pages

Wednesday, October 22, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI AJIFUA KUMKABILI MKENYA HENRY WANDERA NOVEMBA MOSI FRENDS CORNE



Bondia Tomas Mashali  kushoto akijifua wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Henry Wandera kutoka kenya novemba 1 katika ukumbi wa frends corner manzese, akisimamiwa na Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Na Mwandishi Wetu
BON DIA Thomasi Mashali  yupo katika maandalizi mazito ya kumkabili bondia kutoka kenya Henry Wandera Novemba mosi katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

akizungumza wakati wa mazoezi yake juzi Mashali amesema kuwa yupo fiti wakati wowote yeye kufanya kazi hivyo aofii ata kiogo mpambano huo na kuwataka mashabiki wake waje waone anavyo mgalagaza vibaya sana siku hiyo mkenya Wandera

mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayo wakutanisha Mbayo Ilunga na Fred Sayuni wakati Joseph Mbowe ataoneshana umwamba na Saidy Salum na Ramadhani Johncena ataoneshana ubabe na Baina Mazola

na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 7000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

No comments:

Post a Comment