Tangazo

Pages

Monday, July 7, 2014

MTANZANIA COSMAS CHEKA AENDELEZA UBABE WA FAMILIA YA CHEKA NJE YA NCHI YA TANZANIA BAADA YA KUMYUKA BINGWA WA DUNIA WA IBF WA VIJANA ALBINUS FELESIANU NA KUTOKA NAYE SARE NYUMBANI KWAKE NAMIBIA

WINDHOEK, NAMIBIA JULY 7, 2014: Familia ya Cheka ni moto wa kuotea mbali baada ya kuendeleza ubabe wao katika masumbwi baada ya Cosmas Cheka ambaye ni mdogo wake bingwa wa zamani wa IBF/Africa Super Middleweight, Francis Cheka kumwadhibu bila huruma bingwa wa dunia wa vijana wa IBF Albinus Felesianu wa Namibia na kutoka naye sare nyumbani kwake Windhoek, Namibia.

Hata hivyo, matokeo hayo yalipingwa na mashabiki wengi nchini Namibia na kusema kwamba ushindi ulikuwa wa wazi kwa Cosmas Cheka
Mpambano huo uliohudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa ngumi toka nchi za Kusini mwa Africa ulifanyika katika ukumbi wa hoteli ya nyota tano ya Windhoek Country Club Resorts & Casino iliyoko katika mji mkuu wa Namibia Windhoek July 5, 2014.

Cosmas ambaye aliondoka nchini Tanzania mwenyewe bila msaidizi yeyote na wala hakukuwa na Mtanzania mwingine katika pambano lake zaidi ya msimamizi mkuu wa mpambano huo na Rais wa IBF barani Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Onesmo Alfred McBride Ngowi, aliubadilisha ukumbi mzima kuwa wake kwa kushangiliwa na kila mtu bila kujali walikotoka.

Akipigana kwa kujiamini na kutumia staili ya bondia bingwa wa dunia wa zamani Mohammed Ali ya kurukaruka kama kipepeo na kuuma kama nyuki (Fly like a Butterfly, Sting like a Bee.) Cosmas alionyesha kipaji cha hali ya juu cha kuzichapa ngumi.

Aliuanza mpambano kwa kutoka kwenye kona yake ya rangi ya bluu na kuanza kumiminia ngumi za heshima bondia huyo bingwaa wa dunia kwa vijana Albinus Felesianu bila huruma na kuanza kushanguliwa mapema kabisa na mashabiki waliofuatana na  Albinus bila kujali taifa alilotoka. Wengi walisikika wakisema kuwa wanafurahia mchezo wake wa kuvutia na kuwa hawajawahi kumwona bondia kutoka nje kwenda Namibia na kufanya alichokifanya Cheka.

Akisadiwa na kocha wa bondia Bongani Mahlangu kutoka Africa ya Kusini ambaye naye alipigana baada ya pambano la Cosmas na kupigwa na bingwa wa IBF/Afrika uzito wa Lihht “Energy” Abraham Ndaendapo wa Namibia, Cosmas alipigana kama mabondia wengi wa nchini Marekani wanavyopigana.

Mstahiki Meya wa jiji la Windhoek alisimama kumshangilia Cosmas ilipofika raundi ya nane ambapo aliuamsha ukumbi mzima kumshangilia bila kujali kama alikuwa anapigana na Mnamibia mwenzao.
Nayo timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Afrika ya Kusini Banyana Banyana ambayo iliifunga timu ya taifa ya Namibia mchana huo, ilikuwa inaimba nyimbo za kivita wakati Cosmas alimwadhibu Albinus Felesianu na kuufanya ukumbi mzima kuwa sherehe za nguvu.

Jajji wa Namibia Lazarus Nainda alimpa ushindi wa 115 Cosmas na 109 Albinus. Jaji Richard Kabamba - Muya wa Kongo DRC alimpa Albinua ushindi wa 114 na Cosmas 113 na jaji Neville Hotz wa Afrika ya Kusini alitoa sare kwa 114 kwa 114 na kufanya pambano hilo kuwa sare.

Majabali hao wawili vijana watarudiana tena baada ya kipindi cha miezi miwili ili kumpata bingwa kweli wa mkanda wa ubingwa wa IBF Africa, Middle East & Persian Gulf uzito wa Light.
Kuna uwezekano mpambano wa marudiano ukafanyika Tanzania au Namibia kutokana na IBF kutoa nafasi ya kufanyika katika mojawapo ya nchi hizi m

bili.

Mpambano wa ubingwa wa IBF Africa, Middle East & Persian Gulf uzito wa Light uliandaliwa na kampuni ya Warriors Promotions ya jijini Windhoek, Namibia na kudhaminiwa na kampuni ya simu ya Namibia ya Telecom Namibia.

Kamishna mkuu wa mpambano huo alikuwa ni Rais wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzanai Onesmo Alfred McBride Ngowi. Refarii alukwa Herman Gurus-Oab wa Namibia wakati majaji walikuwa Richard Muya wa Kongo DRC, Neville Hotz wa Afrika ya Kusini na Lazarus Nainda wa Namibia.

Cheka alipata marafiki wengi sana kiasi kwamba ilibidi Bodi ya kusimamia ngumi nchini Namibia imwekee ulinzi maalum wa Police ili kumwondelea adha ya kubughudhiwa na mashabiki wengi ambao walikuwa ni wanawake.

Tembelea tovuti yetu ujue mambo mengi kuhusu IBF Africa, Middle East & Persian Gulf katika:

No comments:

Post a Comment