Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Karama nyilawila
ni bondia anayetegemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 may kuzichapa na
Said Mbelwa kuwania ubingwa wa UBO (universal boxing organisation) katika
ukumbi wa friends corner – manzese. Hapo awali karama alikuwa azipige na Thomas
mashali alievunja mkataba wa pambano kwa kutokuwa vema kwa pambano hilo na
badala yake nafasi hiyo ikadondokea kwa said mbelwa ambaye ana vigezo vyote vya
kugombania ubingwa. Karama Nyilawila akiwa katika mazoezi ya mwishomwisho
alisema” Mashali ananiogopa baada ya kusikia mazoezi ninayofanya ni magumu na
hatari kwa bondia atakae katiza mbele yangu, kwani kila siku asubuhi lazima
nikimbie kutoka sinza ilipo gym yetu mpaka kibaha maili moja kwenda na kurudi na
jioni napiga mfuko wa mazoezi(bag) raundi sita za dakika kumikumi na nacheza sparing
raundi 15, aliposikia hivyo mdogo wangu mashali ikabidi achomoe kwa kutafuta
visingizio mbalimbali na pambano limekuwa likibadirishwa tarehe kwa ajili yake
na mwishowe akaweka wazi kuwa ananiogopa.karama aliendelea kwa kusema huyu
mbelwa kavamia adhabu ambayo sio yake,asuburi tarehe ifike apate cha
kumuhadithia mashali.
Nae kiongozi
na mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe amesema siku hiyo pia kutakuwa na
mapambano mengi makali ya utangulizi yakiwemo ya Suleiman tall akizipiga na Abdala pazi,
ramadhan kumbele akimvaa morobest, zumba kukwe wakioneshana ubabe na kamanda wa makamanda, idi athuman na
julias kisarawe.
Wakati huohuo
ndio tunamalizia makubaliano ya mwisho ya bondia chipukizi na mwanamuziki mashuhuri wa bendi ya mapacha watatu Halid
Chokoraa ambae amekubali kuzipiga na Abdul manyenza katika pambano la raundi
nne kilogram 63. chokoraa kwa sasa yupo vizuri sana kwa mchezo wa ngumi na ana
uwezo wa kumkabili bondia yoyote wa uzito wake.
No comments:
Post a Comment