Tangazo

Pages

Saturday, May 31, 2014

COSMAS CHEKA KUTETEA MKANDA WAKE WA UBINGWA LEO JUMAPILI YA JUNE 1


Bondia Cosmas Cheka akipima uzito
  
 

BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana social hall  wa Morogoro
 
Akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kwa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni.
Bondia huyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka  aliyekuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema  yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
 
Pambano hilo linalosimamiwa na TPBO  litasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaeevaana na Sadiki Yusufu,  wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 
 
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic,  Miyeyusho, Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali , Floyd Mayweathar, Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez , Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
  
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ameahidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta, Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakaoonesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi.

No comments:

Post a Comment