BONDIA Ronald Pontillas, atawasili nchini kesho asubuhi kwa ajili ya pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia Francis Miyeyusho, litakalofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa
pambano hilo Mussa Kova, alisema kuwa Pontillas raia wa Ufilipino,
atawasili nchini
akiwa na kocha wake Amogo Samson.
Aidha Kova alisema bondia huyo atawasili majira ya saa moja asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.
''Baada ya kuwasili ataelekea hotelini kupumzika kabla ya saa 5, kuzungumza na vyombo vya habari''. alisema Kova.
Kova alisema kuwa maandalizi mengine yanaendelea vizuri ambapo, suala la viingilio nalo tayari limeshapangwa.
Katika viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni
Katika viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni
sh.20,000 kwa VIP na kawaida itakuwa sh.10,000.
Katika pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambayo yatatangazwa kesho katika mkutano maalum na
vyombo vya habari.
Kwa ujumla maandalizi ya pambano hilo linalosimamiwa na PST Tanzania yanakwenda vizuri.
Kwa ujumla maandalizi ya pambano hilo linalosimamiwa na PST Tanzania yanakwenda vizuri.
"Mabondia wote wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea
Miyeyusho atafanya vizuri na kukabiliana na upinzani wa
mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye kiwango cha
No comments:
Post a Comment