![]() |
Albinus (kushoto) akifanya vitu vyake |
Thursday, February 28, 2013
MNAMIBIA KUUMANA NA MGHANA UBINGWA WA IBF.
Wednesday, February 27, 2013
WATOTO WA NKRUMAH ISSAH SAMIR NA PHILIP KOTEY KUPANDA ULINGONI MACHI 30 KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA MIDDLE
Philip Koyey akichapa makonde na bondia Kelly Brook wa Uingereza.
Nchi
ya Ghana iko katika hekaheka za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa
Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo
gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey.
Mabondia
wawili hao ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na
barani Afrika kwa ujumla, ambao watakutana wakati wanapogombea mkanda wa
IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye 'muziki wa masumbwi' ulingoni
wakati mabondia hao watakapokuwa wakionyeshana umwamba na
kuwadhihirishia mashabiki wa masumbwi katika bara la Afrika kuwa
wanasifa hizo kama wanavyotambulika.
Pambano hilo linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyakula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Makamu wa Rais wa IBF Africa idara ya fedha.
Kwa maana hiyo miamba hiyo inatarajia kukutana na kupanda jukwaani Machi 30,katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah.
Nchi
ya Ghana imetokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti
kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo
imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike
Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa wa ngumi kwa miaka kadhaa na
kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kufuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Tuesday, February 26, 2013
RAMADHANI SHAURI KUZIPIGA 8-03-2013 JIJINI MOSCO -URUSI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-MICHEZO
NDUGU ZANGU WAPENDWA KATIKA MICHEZO ,
NINAYO FURAHA KUBWA SANA NA HESHIMA MBELE YENU KUWAARIFU KWAMBA BONDIA WETU
SHUJAA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA RAMADHANI SHAURI ,BINGWA WA IBF-AFRIKA TAREHE 8-03-2013 ATAPANDA ULINGONI JIJINI MOSCO -URUSI KUZIPIGA NA BONDIA EDUARD TROYANOVSKY ,KATIKA PAMBANO LA RAUNDI KUMI NA MBILI [12]
BONDIA HUYU MTANZANIA ANAONDOKA NCHINI TANZANIA KESHO JUMATANO ALFAJIRI KWA USAFIRI WA BASI LA DAR-EXPRESS KUELEKEA JIJINI NAIROBI KUUNGANA NA WAKALA WAKE NDG FRANKLYN IMENZI TAYARI KWA MAANDALIZI YA MWISHO IKIWA NI PAMOJA NA KUJARIBU KUIZOWEA HALI YA HEWA YA BARIDI YA NAIROBI AMBAYO ANALINGANA KABISA NA HALI YA HEWA YA URUSI.
HII NI MARA YA KWANZA KWA RAMADHANI SHAURI KIZIPIGA NJE YA TANZANIA ,NA TPBO ILIPENDEKEZA JINA LAKE BAADA YA KURIDHIKA NA KIWANGO ALICHONACHO ,
NI KIZURI SANA NA PIA ANAYO NIDHAMU YA HALI YA JUU SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOKUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI IKIWEMO BANGI.
TPBO-LIMITED IMESHAMPATIA KIBALI BONDIA HUYO ILI AKAPAMBANE NA KUONYESHA UWEZO WAKE HUKO RUSSIA ,NA INAMTAKIA MAFANIKIO MAZURI.
KAMA TPBO-LIMITED ILIVYOAINISHA MIKAKATI YAKE KATIKA MWAKA HUU 2013 KWAMBA ITAJITAHIDI KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA MAWAKALA WA NGUMI ZA KULIPWA WA SEHEMU MBALIMBALI ZA ULIMWENGU ILI WAWAPATIE MAPAMBANO MENGI MABONDIA WA TANZANIA,
TUNAMSHUKURU MUNGU KWAMBA MIKAKATI YETU IMEANZA KUZAA MATUNDA.
TAARIFA HII IMELETWA KWENU NAMI
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS -TPBO-LIMITED

Monday, February 25, 2013
IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE MARCH 2
VITA YA UBINGWA WA IBF AFRICA "RICHARD COMMEY NA BILAL MOHAMMED"
Kuna
hekaheka nyingi kwenye jiji la Accra, nchini Ghana wakati wa pambano la
kugombea ubingwa wa dunia kati ya bondia marufu Joseph Agbeko kutoka
Ghana na Luis Mendenez bondia anayetoka katika nchi ya Amerika ya Kusini
ya Columbia watakapokutana siku ya jumamosi tarehe 8 Machi.
Kati
ya mapambano ya utangulizi bondia anayeinukia kwa kasi Richard Commey
atakutana na bondia mwenzake wa Ghana Bilal Mohammed kugombea mkanda wa
IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika
uzito mwepesi (Lightweight).
Wawili
hao wanatoka katika kambi mbili zinazohasimiana kwa siku nyingi na
mpambano wao unategemea kuwa wa kasi, ufundi na wenye kusisimua katika
raundi zote 12.
Mpambano wa Richard Commey (khttp://www.youtube.com/watch?v=IBG5a9LtIhU )
na Bilal Muhammed umekuwa gumzo kubwa katika jiji la Accra pamoja na
majiji mengine katika Afrika ya Magharibi. Hii inatokana na umaarufu wa
promota na meneja wa Ruchard Commey Mghana Michael Amoo Bediako
anayeishi barani Ulaya akiwa na makazi yake nchini Uingereza kuwa mtu
aneyeshughulika na mabondia wenye vipaji vya hali ya juu.
Richard
Commey atapenda kuwadhihirishia wapenzi wake kuwa yeye ndiye Mfalme wa
Afrika katika uzito wa mwepesi (Lightweight) na hakuka atakayeweza
kumzuia katika mipango yake ya kupanda ngazi. Naye Bilal Muhammad
atapenda kuudhihirisia ulimwengu kuwa sio bondia anayeweza kusukumwa
sukumwa na kwamba ubingwa wa IBF AMEPG katika uzito wa Lightweight na
wake.
Imetolewa na:
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Friday, February 22, 2013
MANENO OSWARD ATAMBA KUMCHAKAZA KASEBA MARCH 2
Bondia Maneno Osward akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' akifanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia
Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba walipokutana kwa ajili ya
kuzungumzia mpambano wao utakaofanyika March 2 katika ukumbi wa DDC
Magomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com Na Mwandishi Wetu BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo. “Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D . -- Super D Boxing Coach Email.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania |
Thursday, February 21, 2013
MAKOCHA WA MASUMBWI WAHITIMU KOZI YA HAWALI
Meja Charles Mbuge wa pili kushoto akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Hawari ya ukocha wa mchezo wa masumbwi,Charles Muhilu wakati wa kumalizika kwa kozi hiyo Dar es salaam leo kushoto ni mjumbe wa BFT, Koba Kimanga na Rais wa shirikisho hili, Michael Changalawe.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Baadhi ya makocha wa mchezo wa masumbwi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimu mafunzo ya awali yaliyomalizika Dar es salaam (Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com |
Meja Charles Mbuge akihojiwa na wana habari wakati wa kufunga mafunzo hayo leo |
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi akiojiwa na wandishi wa habari |
kocha Charles Muhilu kushoto akihojiwa kuhusu kozi hiyo |
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi kushoto akiwa na Patric Nyembela wa EATV picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Wednesday, February 20, 2013
Floyd Mayweather alamba mkataba mnono
![]() |
Floyd Mayweather |
BONDIA bingwa wa Dunia mkanda wa WBC Floyd Mayweather Jr ambaye ajawai kupigwa wara kutoka droo rekodi yake won 43 (KO 26)
+
lost 0 (KO 0)
+
drawn 0
=
43 ameingia mkataba wa
kumwezesha kupigana hadi mara sita zaidi ya kipindi cha miezi 30.
mkataba uho mnono utakao mfanya awe mwana michezo wa kwanza duniani
kuingia mkataba mkubwa kuliko mwana michezo yoyote
Mkataba uho utanza kwa mara ya kwanza kwa kupambana na Robert
Guerrero Mei 4 ambapo kuna mfanya awe na mpambano mmoja tangia mwaka
jana mei 5 kumtwanga bondia Miguel Cotto na kuamliwa kwenda jela baada
ya kuitalifiana na mpenzi wake tangia atoke jela ajawai kucheza na ndipo
anapokutana na Robert Guerrero mwenye rekodi won 31 (KO 18)
+
lost 1 (KO 0)
+
drawn 1
=
35
Mkataba huo utausisha matangazo mbali
mbali ya kwenye TV yatakayo muwezesha kumiliki mlungula kwa kwenda
mbele kwa kipindi chote hicho bondia huyo anayekubalika kwa sasa
hususani kwa stayl yake ya kujikinga na kupiga kumi kwa kushtukiza
MCHEZO WA Taichi Kung-fu WAENDELEA KUHAMASISHWA
![]() |
Mkufuzi wa mchezo wa Taichi Kung-fu, Jumanne Wilsoni 'Masta Jumanne'
(kulia) akitoa mafunzo ya mchezo huo Dar es salaam jana katika jengo la
CCM Ilala Dar es salaam jana. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |

Monday, February 18, 2013
MAPAMBANO MAWILI YA IBF AFRIKA KUFANYIKA MWEZI UJAO

Safari
hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama
Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati
bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika
jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal
Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa
wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda
wa IBF Africa katika uzito mwepesi au lightweight.
Wawili
hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa
dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko
atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya
Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Mpambano
mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu
mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick
Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa
wa IBF katika bara la Afrika.
Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
WATOTO WA NKRUMAH WAWANIA UBINGWA WA IBF
Bondia Franisic Cheka kushoto na Thomasi Mashali wakiwa wameushika mkanda wa ubingwa wa IBF Africa watakaogombania mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba wakati wa kutambulisha mpambano huo katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam na Khalid Kibavu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Likiwa limetokea kwenye wiki la mafanikio
makubwa katika majijini ya Johannesburg nchini Africa ya Kusini
na Tunis, Tunisia ambako iyalifanyika mapambano mawili ya ubingwa wa
dunia kwa vijana na ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati, ambako Illunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) aliukwea
ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Cruserweight baada ya
kumsambaratisha Gogito Gorgizadze kutoka nchini Georgia. Aidha bondia
Ayolub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium kumkata ulimi bondia
Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) linajiandaa tena kwa mapambvano mawili makubwa mwezi ujao.
Safari
hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama
Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati
bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika
jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal
Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa
wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda
wa IBF Africa katika uzito mwepesi au lightweight.
Wawili
hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa
dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko
atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya
Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Mpambano
mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu
mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick
Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa
wa IBF katika bara la Afrika.
Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
For Immediate Release Media Contact: Onesmo Ngowi
IBF/Africa Notes 13 Tel: (+255) 754- 360828
Friday, February 15, 2013
DVD MPYA ZA SUPER D BOXING COACH ZINAZOTARAJI KUINGIA SOKONI MWEZI UJAO
![]() |
DVD ITAKAYOHUSISHA MIPAMBANO YA JUAN EMANUEL MARQUEZ |
![]() |
MPAMBANO HUNAO HUSISHA MAHASIMU WAWILI KATIKA MASUMBWI WANAOTAMBA DUNIANI MIGUEL COTTO VS ANTONIO MARGARITO ITAKUWA INAHUSISHA MIPAMBANO YAO YOTE MIWILI NA MINGINE KIBAO |
![]() |
DVD ITAKAYOMUHUSISHA MKALI WA MASUMBWI DUNIANI MANNY PAQUAIO |
DVD INAYOHUSISHA MABONDIA WA TANZANIA AKIWEMO MMBWANA MATUMLA VS FRANSIC
MIYEYUSHO NA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' VS SAID MUNDI NA ROGERS
MTAGWA
MPAMBANO WA MASUMBWI ULIVYOFANYIKA SIKU YA WAPENDANAO
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akipiga picha ya pamoja na Godfrey Silva baada ya kocha huyo kumzawadia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Flana ya SUPER D BOXING COACH Kikingia kinywa na DVD zenye mafunzo ya mchezo wa masumbwi kama zawadi kutoka kwa kocha huyo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Dkt, Milhael Arraham kushoto akimpima Afya Iddy Mnyeke kabla ya mpambano wake na Sadiki Momba jana |
Bondia Cosmas Kibuga kulia akimshambulia kwa makonde Makali mawe wakati wa mchezo wao uliofanyika jana |
Mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kutoka kambi ya Ilala akifatilia mpambao huo |
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Iddyt Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika jana momba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Iddyt Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika jana momba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akioneshana kazi na Shabani Kilumbelumbe wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Kumbele alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mashabiki wa bondia toka kambi ya ilala Iddy Mnyeke wakiwa katika picha ya pamoja na bondia wao |
Bondia Omar Ramadhani akishangilia ushindi baada ya kumpiga Deo njiku kwa point jana na kutawazwa kuwa bingwa wa taifa PST |
Bondia Adamu Yahaya kushoto akipambana na Godfrey Slva wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na PST Silva alishinda kwa Point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ibrahimu Class ' Kking Class Mawe' akifatilia mpambano wa masumbwi uliokuwa ukifanyika manzese Dar es salaam jana na Aasha Kamnyanga ' Mama Iikota' Mrs Super D Boxing Coach. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimkabidhi bondia Godfrey Silva vifaa vya mchezo wa masumbwi ikiwemo Flana, vikingia kinywa na DVD kwa ajili ya mafunzo ya mchezo uho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akipiga picha ya pamoja na Godfrey Silva baada ya kocha huyo kumzawadia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Flana ya SUPER D BOXING COACH Kikingia kinywa na DVD zenye mafunzo ya mchezo wa masumbwi kama zawadi kutoka kwa kocha huyo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Omary Ramadhani kushoto akijaribu kumkwepa bondia Deo Njiku wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Ramadhani alishinda kwa point na kutangazwa kuwa bingwa wa Tanzania PST ,Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Deo Njiku wa Morogoro akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Omary Ramadhani wakati wa kugombania mkanda wa ubingwa wa Tanzania PST Ramadhani alishinda kwa Point .picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia wakisubili matokeo ya mchezo |
Tuesday, February 12, 2013
MASHALI VS CHEKA WASANI KUCHEZA MEI MOSI
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Rais wa TPBO Yassin Abdallah kulia akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa ubingwa Wa IBF kati ya Thomasi Mashali kushoto na Fransic Cheka ayupo pichani katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Franisic Cheka kushoto na Thomasi Mashali wakiwa wameushika mkanda wa ubingwa wa IBF Africa watakaogombania mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba wakati wa kutambulisha mpambano huo katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam na Khalid Kibavu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitia saini mkataba wa makubaliano wa kucheza mpambano na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Promota wa Mpambano wa ubingwa wa IBF Tanaka Adam katikati akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini ya mkataba wa makubaliano wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi mwaka huu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Monday, February 11, 2013
BONDIA IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO
Bondia Ibrahimu Maokola akipiga beg wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia maneno Oswald kulia akimsimamia Ibrahimu Maokola wakati akipiga begi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Saturday, February 9, 2013
DEO NJIKU KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA NA OMARY RAMADHANI February 14
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Deo Njiku wa Morogoro na Omary Ramadhani wataingia uringoni February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese 14 kuwania Ubingwa wa Tanzania PST
Mpambano huo wa aina yake
unatarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana kila mtu kuwa na rekodi nzuri
mpambano uho utakaosindikizwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya Godfrey Silver na Adam Yahya ambapo mipambano hiyo itakuwa ya raundi kumi
Huku
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila 'Super
D' atampandisha kwa mara ya kwanza bondia wake mpya Iddy Mnyeke kuvaana
na Sadiki Momba mpambano utakaopigwa kwa raundi nne
Mgeni rasmi siku hiyo anatsrahjiwa kuwa ni Kamanda
wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela atakaewafisha mikanda ya ubingwa
Super D, alisema katika mpambano huo
atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa
SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na
mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza
watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota
hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali
wengine DVD hizo zina.
michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

Subscribe to:
Posts (Atom)