Tangazo

Pages

Monday, February 18, 2013

MAPAMBANO MAWILI YA IBF AFRIKA KUFANYIKA MWEZI UJAO

Likiwa limetokea kwenye wiki la mafanikio makubwa katika majijini ya Johannesburg nchini Africa ya Kusini na Tunis, Tunisia ambako iyalifanyika mapambano mawili ya ubingwa wa dunia kwa vijana na ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ambako Illunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo
(DRC) aliukwea ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Cruserweight baada ya kumsambaratisha Gogito Gorgizadze kutoka nchini Georgia. Aidha bondia Ayolub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium kumkata ulimi bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana,  Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa)  linajiandaa tena kwa mapambvano mawili makubwa mwezi ujao.

Safari hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda wa IBF Africa katika uzito mwepesi  au lightweight.

Wawili hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.

Mpambano mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika.

Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
 
ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment