Tangazo

Pages

Tuesday, February 26, 2013

RAMADHANI SHAURI KUZIPIGA 8-03-2013 JIJINI MOSCO -URUSI

        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-MICHEZO


NDUGU ZANGU WAPENDWA KATIKA MICHEZO ,

NINAYO FURAHA KUBWA SANA NA HESHIMA MBELE YENU KUWAARIFU KWAMBA BONDIA WETU

SHUJAA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA RAMADHANI SHAURI ,BINGWA WA IBF-AFRIKA TAREHE 8-03-2013 ATAPANDA ULINGONI JIJINI MOSCO -URUSI KUZIPIGA NA BONDIA EDUARD TROYANOVSKY ,KATIKA PAMBANO LA RAUNDI KUMI NA MBILI [12]

BONDIA HUYU MTANZANIA ANAONDOKA NCHINI TANZANIA KESHO JUMATANO ALFAJIRI KWA USAFIRI WA BASI LA DAR-EXPRESS KUELEKEA JIJINI NAIROBI KUUNGANA NA WAKALA WAKE NDG FRANKLYN IMENZI TAYARI KWA MAANDALIZI YA MWISHO IKIWA NI PAMOJA NA KUJARIBU KUIZOWEA HALI YA HEWA YA BARIDI YA NAIROBI  AMBAYO ANALINGANA KABISA NA HALI YA HEWA YA URUSI.

HII NI MARA YA KWANZA KWA RAMADHANI SHAURI KIZIPIGA NJE YA TANZANIA ,NA TPBO ILIPENDEKEZA JINA LAKE BAADA YA KURIDHIKA NA KIWANGO ALICHONACHO ,

NI KIZURI SANA NA PIA ANAYO NIDHAMU YA HALI YA JUU SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOKUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI IKIWEMO BANGI.


TPBO-LIMITED IMESHAMPATIA KIBALI BONDIA HUYO ILI AKAPAMBANE NA KUONYESHA UWEZO WAKE HUKO RUSSIA ,NA INAMTAKIA MAFANIKIO MAZURI.


KAMA TPBO-LIMITED ILIVYOAINISHA MIKAKATI YAKE KATIKA MWAKA HUU 2013 KWAMBA ITAJITAHIDI KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA MAWAKALA WA NGUMI ZA KULIPWA WA SEHEMU MBALIMBALI ZA ULIMWENGU ILI WAWAPATIE MAPAMBANO MENGI MABONDIA WA TANZANIA,

 TUNAMSHUKURU MUNGU KWAMBA MIKAKATI YETU IMEANZA KUZAA MATUNDA.


                    TAARIFA HII IMELETWA KWENU NAMI
                   YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                       RAIS -TPBO-LIMITED

No comments:

Post a Comment