Wednesday, August 31, 2011
NIPO MOROGORO NA MATAARISHO NDIO HAYA
Habibu Kinyogoli juu akijalibu kipande cha ulingo uho baada ya kufunga leo hii maandalizi yanaendelea
KOCHA RAJABU MHAMILA SUPER D AKIWA KATIKA MAPAMBANO YAKE KABLA YA KUA KOCHA
Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila (Super D) kushoto akitangazwa mshindi zida ya bondia Safari Berdard kipindi hicho
Super D Boxing Coach kushoto Akipambana na Rashidi Ali
Super D Boxing Coach kulia akipambana na Ajibu Salumu
Super D Boxing Coach kushoto Akipambana na Rashidi Ali
Super D Boxing Coach kulia akipambana na Ajibu Salumu
Tuesday, August 30, 2011
NGUMI KUPIGWA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO IDI PILI

MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa Middle huku likisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania,(PST).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku katika uzito wa Fly ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia kajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuweza kuibuka na ubingwa ili aweze kuendeleza rekodi yake.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D
MABONDIA WA ZAMANI WATAKIWA KUFADHILI NGUMI

BINGWA wa Mchezo wa kick Boxing nchini Japhet Kaseba amewaomba Mabondia wakubwa kuhakikisha wanaweka na kuchangia fedha zitakazo kuwa zikitolewa kuchangia vyama vya michezo nchini wikiwemo RT na BFT.
Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili leo kwa njia ya simu Gwiji huyo wa Mapigano amesema itakuwa ni jambo zuri kwa mabondia wakubwa kutenga fedha ili kuchangia vyama vya michezo mbali mbali nchini wikiwemo vya Ngumi za ridhaa na riadha badala ya kutegemea nguvu ya serikali tu.
"Sifikili kama tukijaribu tutashindwa japo kwa kiasi kidogo kidogo tuweke mazoea ya kuchangia vyama hivi kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla kuliko kutegemea serikali tu"alisema Kaseba.
Hata hivyo Kaseba amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya All African Games ambayo yanatarajia kurindima hivi karibuni nchini Msumbiji yupo mbioni kuandaa filamu itakayo kuwa ikielezea umuhimu wa kuwekeza katika michezo.
"Lengo la hii filamu ni kujaribu kuwapa hamasa wadau kuwekeza na kuchangia michezo ila pia nataka kuwashirikisha wanamichezo mbali mbali"alisema Kaseba
Monday, August 29, 2011
TIMU YA TAIFA YA NGUMI YAKABIDHIWA VIFAA KUJIANDAA KWENDA ALL AFRICAN GAMES MSUMBIJI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Riadhaa Tanzania,Makore Mashaga akimkabidhi vifaa vya michezo bondia wa timu ya Taifa ya ngumi, Suleiman Kidunda, jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo inayojiandaa kuondoka nchini kuelekea Msumbiji kushiriki katika mashindano ya All African Games. Katikati ni Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Edward Emmanuel.
Sunday, August 28, 2011
TIMU YA TAIFA YA NGUMI YAWA YA KWANZA KWENDA KATIKA MASHINDANO YA 'ALL AFRICA GAME'
Mabondia,makocha pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini wakiangalia DVD zinazotahalishwa na Kocha wa mchezo wa ngumi timu ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala kimichezo, Rajabu Mhamila 'Super D' ayupo pichani ambazo zinafundisha mafunzo ya mchezo huo kabla ya kuondoka kwenda Msumbiji kushirika Mashindano ya 'ALL AFRICA GAME' yatakayoanza mapema wezi ujao timu hiyo ni ya kwanza kwa Tanzania kuondoka leo. (Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)
ZABU JUDAH AGONGA MWAMBA KURUDIANA NA AMIR KHAN
MIPANGO ya Amir Khan imepata kizuizi, baada ya bonsia alipigana naye mara ya mwisho, Zab Judah kutoa malalamiko dhidi ya bondia huyo Mwingereza.
Judah analalamika alipigwa chini ya mkanda wakati katika pambano ambalo alipoteza mkanda wake wa ubingwa wa IBF uzani wa light-welter, ambapo Khan alishinda kwa KO katika raundi ya tano mjini Las Vegas.
Gazeti la The Sun limesema, promota wa Judah ambayo ni kampuni ya Main Events, imekata rufaa katika Kamisheni ya Michezo Nevada na imetuba barua pamoja na ushahidi wa video ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa mataji ya WBA na IBF na inataka kamisheni kuamuru lirudiwe.
Timu ya Judah inadai kuwa refa Vic Drakulich alikuwa hakuona jinsi Khan alivyopiga ngumi chini ya kanda, ambapo alimtangaza kuwa ni mshindi kwa KO.
Timu hiyo imemtuhumu Khan kwa kucheza faulo nyingine katika mechi hiyo.
Rais wa Main Events, Kathy Duva alisema: " Kulikuwa na ngumi zilizokuwa zikipigwa nyuma ya kichwa na kukumbatia na Amir Khan hakuonywa kwa hilo. Video haisemi uongo."
Khan amepanga kupigana na bondia mkongwe wa Mexico, Erik Morales Desemba 10 lakini Judah anatumaini kuwa pambano hilo litazuiwa.
BONDIA JAPHET KASEBA AJIFUA KUMKABILI MANENO OSWARD
Bondia Japhet Kaseba (kushoto) akielekezwa jinsi ya kutupa masumbwi na Kocha wake, Sweet Kalulu wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi yake mwana nyamala ya kujiandaa kupambana na Maneno Osward mwezi ujao katikati ni bondia Kanda Kabongo
MAZOEZI YA KAMBI YA ILALA YANAENDELEA
Mabondia walio chini ya kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa katika mazoezi ya kukaza misuli katika ukumbi wa Amana CCM Dar es Salaam juzi
TIMU YA TAIFA YA NGUMI YAWA YA KWANZA KWENDA KATIKA MASHINDANO YA 'ALL AFRICA GAME'
Mabondia,makocha pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini wakiangalia DVD zinazotahalishwa na Kocha wa mchezo wa ngumi timu ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala kimichezo, Rajabu Mhamila 'Super D' ayupo pichani ambazo zinafundisha mafunzo ya mchezo huo kabla ya kuondoka kwenda Msumbiji kushirika Mashindano ya 'ALL AFRICA GAME' yatakayoanza mapema wezi ujao timu hiyo ni ya kwanza kwa Tanzania kuondoka leo. (Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)
BONDIA ZAB JUDA ALALAMIKA KUPIGWA NA AMIR KHAN
LAS VEGAS, Marekani
MIPANGO ya Amir Khan imepata kizuizi, baada ya bonsia alipigana naye mara ya mwisho, Zab Judah kutoa malalamiko dhidi ya bondia huyo Mwingereza.
Judah analalamika alipigwa chini ya mkanda wakati katika pambano ambalo alipoteza mkanda wake wa ubingwa wa IBF uzani wa light-welter, ambapo Khan alishinda kwa KO katika raundi ya tano mjini Las Vegas.
Gazeti la The Sun limesema, promota wa Judah ambayo ni kampuni ya Main Events, imekata rufaa katika Kamisheni ya Michezo Nevada na imetuba barua pamoja na ushahidi wa video ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa mataji ya WBA na IBF na inataka kamisheni kuamuru lirudiwe.
Timu ya Judah inadai kuwa refa Vic Drakulich alikuwa hakuona jinsi Khan alivyopiga ngumi chini ya kanda, ambapo alimtangaza kuwa ni mshindi kwa KO.
Timu hiyo imemtuhumu Khan kwa kucheza faulo nyingine katika mechi hiyo.
Rais wa Main Events, Kathy Duva alisema: " Kulikuwa na ngumi zilizokuwa zikipigwa nyuma ya kichwa na kukumbatia na Amir Khan hakuonywa kwa hilo. Video haisemi uongo."
Khan amepanga kupigana na bondia mkongwe wa Mexico, Erik Morales Desemba 10 lakini Judah anatumaini kuwa pambano hilo litazuiwa.
BONDIA Robert Helenius ATWAA MATAJI YA WBA NA WBO
MFANO WA KUIGWA EVANDER AWA PROMOTA WA NDONDI
EVANDER NA BINGWA MPYA WA DUNIA UZITO WA JUU WBA
Sunday, August 21, 2011
NGUMI ZAENDELEA KUHAMASISHWA ILALA
Wednesday, August 17, 2011
YOHANA ROBART APANIA KUMDUNDA MKENYA IDDI PILI MOROGORO
BONDIA Yohana Robert ameapa kumsambaratisha mpinzani wake kutoka Kenya James Unyango katika raundi za kwanza la pambano lao.
Pambano hilo linatarajia kuwa katika uzito wa kg 61 katika raundi 6 ambapo litafanyika Sikukuu ya IDD pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni moja kati ya mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya Francis Cheka na Mada Maugo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Yohana alisema, katika mapambano hayo pambano lake ndio linahusisha bondia kutoka nje ya nchi hivyo atajitahidi kuhakikisha ushindi huo unabaki hapa nchini.
"Siwezi kuwaangusha Watanzania na wapenzi wa ngumi kwa ujumla ntahakikisha na msambaratisha mpinzani wangu mapema katika raundi za awali na kuuacha ushindi hapa nyumbani," alisema Yohana.
Alisema, kwa sasa yupo kambini Gongo la mboto chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambapo anajifua ili kuweza kukabiliana na mpinzani wake huyo.
Cheka na Maugo wanarudiana baada ya kushindana kwa pointi moja katika pambano lao la kufunga na kufungua mwaka lililofanyika katika ukumbi wa PTA ambapo Cheka alimzidi Maugo kwa pointi ambapo Maugo alipinga matokeo hayo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao.
DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
Tuesday, August 16, 2011
BFT WAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
MADAKTARI WAKUTANA KUJADILI AFYA ZA WANAMICHEZO
Sunday, August 14, 2011
DVD ZA MAPAMBANO YA NGUMI SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO
DVD ZA MAPAMBANO YA NGUMI KIMATAIFA SASA ZINAPATIKANA KWA WINGI BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM
MABONDIA KUZIPIGA SEPTEMBA 4 MWANANYAMALA
Pambano hilo ambalo litakuwa la raundi nane litasindikizwa na burudani kutoka katika kundi la 'Makhirikhiri wa bongo' huku likitanguliwa na mapambano manne ya utangulizi ambapo yatafanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma wa Mwananyamala Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright' alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka wadau wa mchezo wa ngumi kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mapambano hayo.
Bigright aliyataja ambambano ya utangulizi ni kati ya Anthon Mathias na Shabani Madilu ambapo pambano lao litakuwa la raundi sita.
Wengine ni Joseph Mbowe na Ezekiel Ezekiel raundi nne, Isa Omari na Kade Hamis raundi sita na Sadat Miyeyusho na Herman Richard raundi sita.
Pia wamo Yona Miyeyusho na Haruna Said raundi nne, Martine Richard na Jumanne Kilumbelumbe raundi nne na pambano la mwisho litakuwa kati ya Mwaite Juma na Franck Pury raundi nne.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao.
DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
BFT YAWEKA HADHARANI WATAKAOWAKILISHA ALL AFRICA GAMES
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) kwa kushirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo Raia wa Cuba Hurtado Primentel imechagua na kuwatangaza mabondia nane watakaoiwakilisha nchi katika michuano ya Mataifa ya Afrika 'All Africa Games' itakayoanza Septemba 3 mwaka huu, Maputo Msumbiji.
Mabondia hao ni Leroi John kg 52, Emilian Patrick kg 56, Nasser Mafuru kg 60, Victor Njaiki kg 64, Joseph Martine kg 69, Seleman Kidunda kg 75, Haruna Swanga kg 91 na Maximilian patrick 91+.
Akizungumza Akiwa Kibaha, Pwani Katibu MKuu wa BFT, Makore Mashaga alisema mabondia hao tayari wameanza kambi jana katika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha.
"Hivi ninavyokwambia tupo njia (jana) tukielekea Kibaha, Pwani kwa ajili ya kuwapeleka mabondia wetu tayari kwa kuanza kambi yao ambayo itadumu hadi siku ya kwenda Maputo,"alisema Mashaga.
Alisema mabondia wote waliochaguliwa ni wenye uwezo mkubwa utakaoweza kuiletea sifa nchi kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika na kwamba ni matarajio ya BFT mabondia hao watazingatia yale watakayoelekezwa na walimu wao.
Alisema kambi hiyo ina jumla ya watu 10 huku mabondia wakiwa nane pamoja na makocha wawili, Hurtado na kocha mzawa ambaye ni msaidizi wa Hurtado Edward Emanuel.
Mashaga alisema kambi hiyo inagharamiwa na kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kwamba msaada uliotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa sh. milioni 3 utasaidia kuboresha masuala mazima ya kambi hiyo.
Ngumi ni miongoni mwa michezo sita iliyochaguliwa na Serikali kuiwakilissha nchi kwenye michuano hiyo ambapo michezo mingine ni riadha, Netiboli, Soka, PARALIMPIKI na Judo.
WANAWAKE KUAMASISHA NGUMI IDI PILI MORO
MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika siku ya Idd pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa katika raundi 10 uzito wa Kg 72 huku likisimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa (PST).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku likiwa katika uzito wa kg 52 ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia anaendelea kujifua katika gym yake tayari kwa kusubiri siku hiyo ambapo maandalizi yanaendelea.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo hapo uwanjani na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
WADAU WA MASUMBWI WAOMBWA KUJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA
WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini wameombwa kujiandaa na kuhudhuria kwa wingi mkutano wa wazi wa kimataifa kuhusu mchezo huo utakaofanyika Agosti 18 hadi 21 Lusaka nchini Zambia.
Mkutano huo umedhaminiwa na Muungano wa Vyama vya Ngumi Afrika, unaofahamika kama African Boxing Union (ABU) na kuandaliwa na wenyeji wa mkutano kupitia Chama cha Ngumi Zambia (BBZ).
Akizungumza na Majira kwa simu juzi akiwa mjini Iringa, Makamu wa Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) ambao ndio waratibu wa mkutano hapa nchini, Dkt. Fistus Luisa alisema utashirikisha pia semina ambao hawana mafunzo ya kutosha.
"Hii ni nafasi kubwa sana kwa wadau wa mchezo wa ngumi barani Afrika kujifunza kupunguza matatizo tuliyokuwa nayo katika kila eneo linalohusu ngumi, tunawaomba wadau wakiwemo makocha, waamuzi, mabondia wa sasa na wazamani na vyama mbalimbali tujiandaae tukashiriki.," alisema.
Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chama cha ndondi nchini humo gharama za kwenda na kurudi hoteli na matumizi mengine zinafikia kiasi cha dola 600 ambazo ni sawa na 8,40,000 za kitanzania.
Makamu huyo alisema mkutano utahudhuriwa na Rais wa ABU ambaye pia ni makamu wa kwanza wa raisi wa Chama cha Dunia cha mchezo wa ngumi WBC, Hausin Hauchi, Katibu mkuu wa ABU ambaye pia ni Rais wa chama cha ngumi cha Uganda (UPBC), Selestino Mindra.
Alisema TPBO inaratibu maombi ya wadau watakaohudhuria au katika anwani ya chama cha ngumi cha Zambia ambao ni waandaaji ambapo mwisho wa kuthibitisha kushiriki ni Julai 30 mwakja huu.
Akizungumzia mkutano huo Rais wa TPBO, Yassin Abdallah 'Ustaadhi' alisema ni mhimu kwa nchi kama Tanzania kutokana na mchezo huo kuanza kupoteza imani kwa nchi tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Tunatambua kuwa watanzania walio wengi hali ya kifedha sio nzuri lakini nawahakikishia mkutano huu ni mhimu sana na watakaothubutu kuhudhuria watakuwa wamepata darasa kiasi kwamba ujuzi wao utaongezeka.," alisema Yassin.
Saturday, August 13, 2011
MAZOEZI YA NGUMI KAMBI YA ILALA
Kocha wa ngumi Habibu Kinyogoli akimwelekeza jinsi ya kutupa masumbwi bondia Maliki Kinyogoli wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)