Tangazo

Pages

Tuesday, August 30, 2011

NGUMI KUPIGWA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO IDI PILI

 


MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.

Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.

Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa Middle huku likisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania,(PST).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku katika uzito wa Fly ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.

"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.

Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia kajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuweza kuibuka na ubingwa ili aweze kuendeleza rekodi yake.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D

No comments:

Post a Comment