Tangazo

Pages

Wednesday, July 20, 2016

KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KUSHILIKI BONANZA VINGUNGUTI JULAI 30



Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabondia watakaoshirika katika bonanza la michezo mbalimbali litakalofanyika Vingunguti kiembembuzi julai 30 kwa ajili ya kuamasisha mchezo uho Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Idd Mkwela kushoto na Vicent Mbiliyi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya 'Super D Coach Uhuru GYM' Kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Idd Mkwela kushoto na Vicent Mbiliyi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya 'Super D Coach Uhuru GYM' Kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA kutoka katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM , iliyopo kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini julai 30 mwaka uhu mabondia wake watashiriki katika bonanza maalumu walilo alikwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini

mabondia hawo watakaoshiliki ni Ibrahimu Class .Idd Mkwela, Vicent Mbilinyi, Fadhili Boika,Mohamed Kisua,Shabani Kaoneka, Gasper Mseveni ambao watacheza siku hiyo

Bonanza ilo lililo ratibiwa na mwenyekiti Moses Mwakibolwa pamoja na wajumbe wake Alli Bakari 'Champion' Spear Mbwembwe ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu

akizungmzia bonanza hilo mmoja ya wajumbe Alli Bakari amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuwatoa vijana kwenye makundi ya vijiweni uharifu pamoja na utamiaji wa madawa ya kulevya

Bonanza hili lililopewa jina la 'Hapa Kazi 2016' litafanyika nchi nzima lakini kwa kuanzia wameanza na wilaya ya Ilala 

pia kufanikisha jambo hili wamejipanga kushirikiana na tasisi mbalimbali ikiwemo kupata ufadhili wa makampuni pamoja na bank mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha vijana wote wanakutanishwa katika michezo na kuelimishwa jinsi ya kufanya kazi

siku hiyo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo ndondi mpira wa miguu kuvuta kamba kukimbiza kuku kwa wazee mpira wa pete kwa wasichana dhuna draft na michezo yote kwa ujumla

pia kutakuwa na zawadi ndogo ndogo kwa washiriki watakaofanya vizuri siku hiyo  

No comments:

Post a Comment