Wapo wanamichezo
waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa
ndondi.
Miongoni mwa
wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield,
Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Mchezo wa ngumi katika nchi
yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi kutokana na kuchipukia kwa mabondia
wengi na mapromota ambao wanapigana katika kuwania mataji mbalimbali nje
na ndani ya Tanzania na kuandaa mapambano . wapo mabondia wengi katika
historia ya Tanzania ambao wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza
kuhusu ubora wa mchezo wa ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo
ndani ya nchi yetu ni imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami
kuwa bado unahitaji vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .
Kwa
Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje ya
Tanzania kama Stanley Mabesi 'Ninja' Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa ,Habibu Kinyogoli Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi na ni mwanaharakati wa mchezo uho kwa nyanja zote kwa sasa
na Emanuel Mlundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo
huo.
jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa
kumbi bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu
wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini nimeona nijaribu kulitilia mkazo .
Natoa mfano kama
tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani
zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil Ivory Coast na nyingine basi hata mchezo wa ngumi
linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa
kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea kumbuka
silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.
Kwa
Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO,KBF bila
kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga
katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo
ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa mchezo
huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa mpira wa
miguu ambao hata mchezo wa kufukuza upepo Riada wanafaidika nao halikadharika
wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka mchezo
wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama ilivyo Las
Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri inawezakana kwa
Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama vya mchezo wa ngumi
vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana na serikali kupitia
wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha tunapata kumbi bora ya
kisasa ya kupigania ili kuongezea ujuzi na viwango vya mchezo wa ngumi
kwa Tanzania.
Kama Ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata
Tanzania inaweza pia kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo
pekee ambao unakuja kwa kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania
Nina maliza kwa kusema kuwa ni imani
yangu kuwa kwa kujengwa uwanja huo kutawapa mabondia wa tanzania
kujiaamini na kuupanua mchezo huo na unaweza pia kulitangaza jina la
Tanzania katika Nyanja za utalii ndani na nje ya Tanzania kama
inavyowezekana kuleta mastaa wakubwa wa muziki kutoka ulaya na amerika
ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa Tanzania .
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa
zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Floyd Mayweather, akifuatiwa na Manny Paquaio
mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania,
Cristiano Ronaldo.
Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James,
wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi
akishika nafasi ya tano,
nina mengi ya kuongelea kuhusu mchezo wa masumbwi hila kwa leo naomba nishie hapo
Na: Super D Boxing Coach www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' |
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.com www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255713 406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
No comments:
Post a Comment