![]() BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
bondia huyo mtanzania anaefanya
shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya
mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
na akishinda mchezo uho
itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa
wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na
mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii
ya feb 26
Kimweri alitoa shukrani za
kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka
sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni
Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli ,
Rajabu Mhamila 'Super D'
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
ambao amekuwa chachu katika
mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama
anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake
ndipo kilipozikiwa
|
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kocha wa Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini |
Friday, January 29, 2016
BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIA
MABONDIA KUTWANGANA DAR LIVE MARCH 12
Mabondia Iddi Mnyeke kushoto na Mohamed Kashinde wakiangaliana kwa usongo wakati wa utambuklisho wa mpambano wao utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA mbalimbali watazitwanga march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala akizungumza mbele ya waandishi wa habari mratibu wa mpambano uho
Rajabu Mhamila 'Super D' amewasainisha mabondia mbalimbali kuzipiga siku hiyo ambapo bondia Ibrahimu Maokola 'Simba wa Mbagala' atazipiga na Joseph Sinkala kutoka Mbeya mpambano wa ubingwa raundi kumi kg 74 utakaosimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa 'TPBC' kinachongozwa na Rais Chaurembo Palasa
aliendelea kwa kusema siku hiyo bondia Iddi Mnyeke kg 61 atamenyana na Mohamed Kashinde wakati Pius Kazaula kutoka Morogoro atakumbana na Karage Suba katika uzito wa kg 66
wakati Shabani Kaoneka atakumbana na Said Seleman mpambano wa raundi sita kg 72 na Ambokile Chusa atavaana na Seleman Galile katika mpambano wa raundi sita kg 74
pia kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayo sindikiza mpambano uho
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania
MAYWEATHER, PACQUIAO
WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA
Pacquiao na Mayweather
Mayweather akisalimiana na Manny Pacquiao
Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameudhihirishia ulimwengu
kuwa uhasama uliopo kati yao ni wa ulingoni na sio sehemu nyingine, hiyo
ni baada ya kukutana uso kwa uso na kusalimiana kama vile sio mahasimu
wakubwa.
Mabondia hao wanaoshikilia mataji makubwa ya ndondi, walikutana katika
uwanja wa American Airlines usiku wa kuamkia leo(Jan27) wakati wa mchezo
kati ya timu ya mpira ya Miami Heat na Milwaukee Bucks katika mchezo
uliomaliza kwa Bucks kushinda kwa jumla ya vikapu 109 – 102 dhidi ya
Heat.
Mbali na mchezo huo, mashabiki na wapenzi wa masumbwi Duniani kote
wamekuwa wakisubira kwa hamu mpambano wa wawili hao ambao wamekuwa
wakitambiana kwa kipindi kirefu unaotajwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.
Watazame hapo chini wakisalimiana
Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
2FACE ANASWA NA MCHEPUKO
Mwanamuziki wa Nigeria, Innocent Idibia ‘2face’ amejikuta katika wakati
mgumu baada ya picha zinazomuonyesha akifanya mambo ya chumbani na
mwanamke mwengine katika klabu yake ya usiku kuzagaa kama njugu kwenye
mitandao mbalimbali.
2face na Annie siku ya harusi yao
2face na Annie siku ya harusi yao
Kwa mujibu wa tovuti moja ya udaku nchini humo, imedai mwanamke
anayeoneka katika picha hiyo ni mama wa watoto wa tatu wa 2face
anayeitwa Pero Adeniyi, ambaye amekuwa akipigwa vita mara kwa mara na
mke wa ndoa wa mwanamuziki huyo ‘Annie Idibia’ aliyezaa nae watoto
wawili wa kike.
2face mwenye umri wa miaka 39, ameamua kuzima soo hilo kwa ku-post picha
kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mke wake katika siku yao ya
harusi na kuwataka watu wasipende kuingilia mapenzi yao kwani watakuja
kuujua ukweli na utawaweka huru.
”Our love does not have 2 make sense 2 u. pls go on with your perfect
life and know the true story behind something before u judge and start
making nasty comments based on an orchestrated story by some blog.U
shall know the truth and the truth shall set u free.LYTID uwana
idibia”,aliandika 2face
2face Idibia
2face na katika mapozi tofauti ya kimahaba na mzazi mwenzie,Pero
Adeniyi.
Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
MAGAZETI YA LEO ALHAMISI
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08790
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08804
.
.
.
.
DSC08807
.
.
.
DSC08811
.
.
.
.
.
DSC08810
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
Newer Posts Older Posts Home
Wanaotembelea Blogu hii
Sparkline 2141575
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI
BOFYA HAPA KUTAZAMA
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA
Tanzania National Flag
Tanzania National Flag
Time
Dar es Salaam
The Digital Company
The Digital Company
Mtayarishaji:
Mtayarishaji:
Richard Mwaikenda
BONGO HITS
Find more music like this on GongaMx
Blog Archive
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Monday, January 25, 2016
BONDIA FRANSIC CHEKA ATUA NCHINI NA KUMPIGIA MIKWALA MSERBIA GEARD AJOTOVIC
Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia
Geard Ajetovic kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa
habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo
aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia
Geard Ajetovic kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi
wetu
Dar es
Salaam. Bondia Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia
Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la
uzito wa super middle la Shirikisho la
Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF).
Cheka na
Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano
lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.
Akizungumza
jana, Cheka alimpongeza meneja wake,
Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka
kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa
upande wake.
Alisema kuwa
Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya
kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye
mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.
“Kwanza
naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii,
nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu
mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa
nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote
duniani,” alisema Cheka.
Alisema kuwa
kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku
akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.
Meneja wa
Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced
Security Limited alisema kuwa lengo la
kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za
kulipwa hapa nchini.
Ndambile
alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho
kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna
mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao
watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa
ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa
wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde
pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.
|
Sunday, January 24, 2016
BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI
VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016 |
Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa aji ya kuwasambalatisha mabondia wengine watakaopita mbele yake
bondia huyo mpaka sasa ameshacheza michezo tisa na kushinda 7 kupoteza na droo 1 ambapo imemuweka katika rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana
akizungumza na mwandishi wa habari hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D'
aliendelea kwa kusema kuwa nilingia katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo
nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake wa kutoka katika mchezo wa ngumi
na naisi katika uzito wake kwa sasa akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao wanatamba na waliotamba
Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwatafutia mipambano mbalimbali ya nje na ndani
MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI
Bondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kutia saini za makubaliano ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri |
Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74
akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo
aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini
ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa 'ring' la ngumi ata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hiro kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili zisonge mbele
siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Wednesday, January 20, 2016
MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO
Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Shsharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS |
KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU |
Promota wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA Na Mwandishi Wetu MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59 akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni na Baina Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengipia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha |
Monday, January 11, 2016
MCHUMIATUMBO ASAINI KUPIGANA NA BENK MWAKALEBELA JANUARY 30
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebelajanuary 30 katika ukumbi wa sativa Kyela Mbeya mpambano uho wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa uho
akisaini mkataba uho mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito uho
Juma Urungu 'Mkebezi'
ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano uho
nae Rais wa TPBC Chaurembo Palasa ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo uho wa masumbwi nchini
kwanza wata akikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama wa mabondia wenyewe na usalama wao wawapo mchezoni
aliongeza kwa kusema kuwa watapima afya siku tano kabla ya mpambano huo ili kujilidhisha na afya za mabondia hawo wenye uzito wa juu nchini ambapo mabondia hawo wamekuwa adimu sana hapa nchini
BONDIA MCHUMIATUMBO KUMKABILI BENK MWAKALEBELA JANUARY 30 KYELA MBEYA
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kulia akisoma mkataba wake na kocha wake Juma Urungu 'Mkebezi' |
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akizungumza na promota juu ya mpambano wa Alphonce Mchumiatumbo katikati |
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akimpatia kiasi cha fedha bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto ni |
Bondia Alphonce Mchumiatumbo akisaini mkataba wa kupambana na Benki Mwakalebela January 30 |
Friday, January 8, 2016
MABONDIA KAONEKA NA MAPAMBANO KUZICHAPA FEB 14 TANDIKA
Mabondia Shabani Kaoneka kushoto akitunishiana misuli na Imani Mapambano baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe katikati ni mdau wa mchezo wa masumbwi Zahoro Maganga 'Super Diego' picha na SUPER D BOXING NEWS |
picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Shabani Kaoneka na Imani Mapambano wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya feb 14 uzito wa kg 74 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe
mpambano huo wa raundi nane utasimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'ostadhi' mpambano huo wenye kugombaniwa kwa kila mmoja kuwa juu ya mwenzie ambapo bondia Kaoneka ni namba 11 katika viwango vya ubora nchini ambapo amepigana mapambano 13 akishinda 5 kupigwa 5 na sale 3
atakuwa na kibarua kizito cha ku lilia namba yake kwa mtu wa chini yake Imani Mapambano anaeshikilia nafasi ya 12 ya ubora kwa mabondia wa Tanzania akiwa amecheza mapambano 7 akishinda 4 na kupoteza 3
katika mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Hassan Mwakinyo atakae pambana na Salumu Salumu kg 72 katika mpambano wa raundi sita
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Sunday, January 3, 2016
CHEKA KUPANDA URINGONI FEB 23 DAR ES SALAAM
Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' pamoja na Meneja msaidizi wa bondia Faransic Cheka Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa
oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi'
pamoja na Meneja msaidizi wa bondia Faransic Cheka Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Saturday, January 2, 2016
MABONDIA WATIFUANA KATIKAS KUFUNGUA MWAKA
Mabondia Shedrack Ignas kushoto akipambana na Abdallah Luwanje wakati wa mpambano wa kufungulia mwaka uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Luwanje alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Abdallah Luwanje akinyooshwa mkono kuashilia ushindi |
Bondia Hassani Mgos kushoto akipambana na Hassani Kitango wakati wa mpambano wao Kitango alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Hassan Kitango akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi |
Mohamed Kashinde akipambana na Mwinyi Mzengela masbondioa hawo walitoka droo |
matokeo ni drooo |
Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
MABONDIA KUNYUKANA LEO MANZESE FRENDS CORNER
Mabondia Mwinyi Mzengela akitunishiana misuli na Mohamed Kashinde baada ya kupima uzito jana kwa ajili ya mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Shomari Milundi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wa leo kushoto ni mpinzani wake Hussein Mbonde mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Subscribe to:
Posts (Atom)