Tangazo

Pages

Friday, January 29, 2016

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIA







BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippines mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title  utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho 
 
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA 
 
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 
na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26
 
Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D' 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa
 
 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi  kocha wa  Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto)   kocha   Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

No comments:

Post a Comment