BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibada Lizbeth Sivhaga wa nchini humu
huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awali
ata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili
ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote
bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne
Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi |
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili |
No comments:
Post a Comment