NA MWANDISHI WETU

KUNA kitu wengi hawakielewi kuhusu Floyd Mayweather Jr. Tangu aanze
kucheza ngumi za kulipwa hajawahi kupoteza, lakini tangu aanze kupanda
ulingoni amepigwa mara moja tu na aliyeifanya hii kazi anapatikana
katika mji wa Pazardzhik, Bulgaria. Unamjua ni nani?
Anaitwa Serafim
Rorodov. Kwa kumtazama usoni hivi sasa inaweza ikawa ngumu kwako
kuamini ulichokisoma hapo juu, lakini ukiyapitia vizuri mashindano ya
Olympic mwaka 1996 yaliyofanyika Atlanta, Marekani utatikisa kichwa
chako na kutoa heshima kwake.
Kwa sasa Todorov anaishi pamoja na
mke, mtoto wake wa kiume na binti wake wa kike ambaye ni mjamzito.
Maisha yake ni ya chini mno na hakuna kilichobora kwenye maisha yake
zaidi ya rekodi ya kumchapa kisiki Floyd Mayweather japo mwenyewe
amekuwa akichukizwa mara kwa mara kila anapokumbushiwa suala hili.
Kwanini? Ilikuwa akampiga Mayweather? Makala haya yamekusanya majibu
yote ya maswali hayo.
Ushindi wa Todorov alioupata enzi hizo akiwa
na umri wa miaka 27 mbele ya Mayweather aliyekuwa na miaka 19 kwenye
pambano la uzito mwepesi katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya
Olympic mwaka 1996, ndio pigano la mwisho Mayweather kupoteza ulingoni.
Miezi michache baadae baada ya kichapo hiko, Mayweather aliachana na
ngumi za ridhaa na kuingia kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa
alipotengeneza rekodi ya kucheza michezo 47 bila kupoteza mpaka sasa na
kutengeneza mamilioni ya pesa.
Kwa Todorov mwenye miaka 45 sasa,
kuna tofauti kubwa ya kimaisha baina yake na Mayweather tangu mara ya
mwisho wawili hawa walipopambana.
Mayweather aliyepoteza pambano
anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 280 wakati Todarov
aliyeibuka kidedea hamiliki hata ‘flat screen’ sebuleni kwake. Hali hii
ndio inayomtia simanzi Todorov kila siku.
Kwa kipindi kirefu
mashabiki wa masumbwi hususani Wamerakani wamekuwa wakiuponda ushindi wa
Todorov wakidai kuwa majaji wa pambano lao walimpendelea.
Lakini
hili ni kama halimuumizi kichwa sana Todorov, kinachoonekana kumtatiza
ni namna maisha yake yalivyobadilika tangu alipotoa kichapo hiko cha
Kihistoria miaka 19 iliyopita.
Mikosi ilianza kumuandama baada ya
pambano lile ambapo Todorov alitemwa na shirikisho la masumbwi hali
iliyomfanya ashindwe kuliwakilisha taifa lake katika mapambano ya
kimataifa.
Wakati leo hii Mayweather akijiandaa kupokea dola milioni
180 kwa pambano lake dhidi ya Pacquiao, Todorov anaishi kwa kutegemea
pensheni ya dola 435 kwa mwezi.
Hali hii inamfanya Todorov,
binadamu pekee aliyemchapa Mayweather ulingoni kuamka kila siku asubuhi
na kujuta kwanini alishinda pambano hilo.
“Alikuwa na miaka 19
kumbuka, uzoefu wangu ulingoni ulikuwa mkubwa zaidi yake. Nilishawachapa
mabondia mbalimbali kutoka Urusi, Cuba, Ujerumani, Ufaransa na
Uingereza” alisema Todorov
“ Lilikuwa pambano zuri na la kuvutia,
unahitaji kuwa vizuri zaidi ya mwenzako ili kupata ushindi. Mimi
nilikuwa vizuri kwa siku ile”aliongeza bondia huyo.
Todorov bingwa
mara mbili wa Ulaya katika ngumi za ridhaa alianza kujifunza ngumi akiwa
na miaka 8 akipata mafunzo kutoka kwa mjomba wake katika kitongoji cha
Peshtera, kusini mwa jiji la Pazardzhik, Bulgaria.
Udhaifu pekee wa
Todorov ambao kocha wake Georgi Stoimenov, aliueleza ni kuwa, mbali na
uhodari wa bondia huyo ulingoni ni mbovu sana kwa wanawake.
“
Tukiwa kwenye mashindano, kocha unatakiwa kulala chumba tofauti na
kijana wako. Lakini kwangu ilikuwa lazima nilale nje ya mlango wa
Todorov kwa ajili ya kumlinda” alisema kocha huyo.
Stoimenov
aliongeza kuwa kuna kipindi alilazimika kumfungia Todorov kwa nje,
lakini alipoamka asubuhi alimkuta ametoroka chumbani kwa kupitia
dirishani.
Unajua Stoimenov alimpatia wapi Todorov? “ alimkuta mklai
huyo akiwa amejifungia kwenye kambi ya wanawake waliokuwa wakishiriki
riadha.
Hatahivyo Todorov anakubali kuwa Mayweather ni bondia mkali
lakini kwa upande wake hakutumia muda mwingi kumchunguza kabla ya
kupanda nae ulingoni.
“ Nilikuwa bondia niliyekamilika sana. Sikuwa
na muda kumsoma. Nilipomtazama ulingoni kwenye pambano lake la robo
fainali, ilitosha sana kwangu kuona udhaifu wake na kumchapa” alisema
Todorov.
“ Lakini ukweli halikuwa pambano la kawaida, nilimpiga mmoja kati ya mabondia bora kabisa ulimwenguni.” Aliongeza Todorov.
Kuhusu hali ya maisha yake ilivyo hivi sasa, Todorov amekiri
kuvurugika na akichukua zaidi kuwa na rekodi hiyo ambayo kwa sasa dunia
inamtazama kwa sana.
“ Kwenye maisha, ni kawaida kushinda vitu
vichache na kushindwa na vitu vingi. Nachukia na ninajutia kuwa na
rekodi ya aina hii kwenye maisha yangu” alisema Todorov.
Sababu
kubwa inayodaiwa kusababisha mapromota kumkumbia Todorov na kuanza
kuweka pesa kwa Mayweather, ni kitendo cha mkali huyo kudengua mara kwa
mara katika kusaini mikataba.
Lakini mmoja wa watu waliokuwa
wakifanya kazi na bondia huyu, Angel Angelov, anasema kuwa maisha ya
Todorov yalibalika tangu alipopokea kichapo kutoka kwa Kamsing.
Angel anaamini kuwa Todorov bado ana mawazo ya pambano lile ambalo
aliamini ni wazi kuwa majaji walimkandamiza ili apoteze pambano lile.
“ Nakumbuka Todorov alikuwa karibu ya kuchanganyikiwa baada ya raundi
ya kwanza ya pambano lile. Alifoka kwa hasira kwa kocha wake akimwambia
kuwa majaji hawahesabu ngumi zake” alisema Angel ambapo mwisho wa siku
Todorov alipoteza pambano hilo kwa pointi 8-5.
Baada ya kichapo hiko, Todorov alitumia siku mbili akiwa hotelini akisubiri ndege ya kumrudisha kwako.
“ Sitaacha kunywa pombe kwa maisha yangu yote, na ninataka kifo change
kinikute nikiwa na pombe” alisema Todorov anayehisi maisha yake
yametawaliwa na usaliti.
Kwa sasa Todorov anaishi katika kibanda
kilichozungukwa na mashamba ya ya ndizi eneo linalofahamika zaidi
kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini Bulgaria.
“
Kuna mambo ya ajabu zaidi mahala hapa, mambo mengi mabaya yanaendelea
mahala hapa. Sipendezwi na maisha haya. Hakuna sehemu za mafunzo ya
ngumi za kutosha, siongei na watu wengi wa hapa na kwa sasa sihitaji
zaidi marafiki. Nahitaji kupumzika tu” alisema Todorov.
Todorov
anaamini kama angepoteza pambano lile la Mayweather, angeendelea vyema
na mchezo huo kama alivyofanya kwenye michuano ya Olympic.
Pia
anaamini kabisa asingepata nafasi ya kuishi Marekani alikokutana na
fedheha ya kichapo cha uonevu mbele ya Kamsing. “ Yameshatokea, na
nimeshasahau. Kwa sasa nahitaji kuishi na kusahau yaliopita. Kuna mambo
ya kipuuzi niliyafanya na nilipokuja kugundua tayari nilishadumbukia
shimoni”
Kuhusu rekodi yake ya kumchapa Mayweather kama bado watu
wanaikumbuka, Todorov alisema “ Wanakumbuka, lakini huwa sipendi kusikia
ninapopota mtaani watu wakisema, Yule ndiye mtu aliyewahi kumpiga
Mayweather”.