Tangazo

Pages

Saturday, April 25, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI 'SUGU' AJIFUA KUMKABILI KEIS AMAL MEI 30


 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi 'Sugu'  ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake mwingine utakaofanyika mei 30 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba ambapo atakabiliana na Keis Amal kutoka Mzazi GYM

bondia huyo anaenolewa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ameingia kambini jana kwa ajili ya mpambano uho wa raundi sita ambapo siku hiyo mpambano mkubwa utakuwa ni kati ya bondia Fransic Cheka na Kiatchai Singwancha . kutoka
Thailand


mpambano utakaokuwa wa raundi kumi promota wa mpambano uho Kaike Siraju aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ya kuvutia ambayo yatatajwa wakati ukifika 

hata hivyo amendelea kumkumbusha Cheka kuwa afanye mazoezi ya kutosha na akumbuke bondia anaekuja kucheza nae ni zaidi aliwo kutana nawo awali

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Bondia Vicent Mbilinyi 'Sugu' kushoto akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya Mbilinyi kujiandaa kupambana na Keis Amal  mpambano utakaofanyika mei 30 katika ukumbi wa P.T.A sabasaba Dar es salaam Picha na
SUPER D BOXING NEWS


Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255713406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment