Tangazo

Pages

Wednesday, June 5, 2013

MASUMBWI KUPIGWA TENA TAIFA

     TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-MICHEZO

NINAYO FURAHA KUBWA SANA KWENU KUWA PAMOJA TENA KATKA KUHABARISHANA MAMBO YANAYOJIRI KATIKA TASNIA YA MASUMBWWI YA KULIPWA NCHINI,

KAMA MNAVYOFAHAMU KWAMBA TPBO-LIMITED IMEKUWA IKIKABIDHIWA NA MAPROMOTA  MAJUKUMU YA KUSIMAMIA NA HATA KURATIBU MATUKIO MABKUBWA YAHUSUYO MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA HAPA NCHINI TANZANIA.

NI JAMBO LA KUJIVUNIA SANA KUONA KWAMBA MAPROMOTA WENYE UWEZO WA KUANDAA MATUKIO MAKUBWA  WANAIAMINI SANA KAMPUNI YETU YA TPBO-LIMITED.

SASA NAWAARIFU KWAMBA KAMPUNI MAARUFU INAYOMILIKI VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NA WAANDAAJI WAKUBWA WA MATAMASHA MAKUBWA YA BURDANI YAKIWEMO YA KIMATAIFA -GLOBAL PUBLISHERS-LIMITED WAMPETUKABIDHI JUKUMU LINGINE KUBWA LA KITAIFA LA KURATIBU MAPAMBANO YA NGUMI ZA KULIPWA YATAKATOFANYIKA KATIKA UWANJA MKUU WA TAIFA HAPO TAREHE 07-07-2013 KATIKA TAMASHA MAARUFU SANA LIJULIKANALO KAMA USIKU WA MATUMAINI  [NIGHT OF HOPE].

KWA KUWA TAMASHA HILI NI KUBWA NA LENYE LENGO LA KUSAIDIA KUCHANGISHA PESA AMBAZO ZITATUMIKA KUSAIDIA UJENZI WA MABWENI YA AKINA DADA ,NASI TPBO HATUNA BUDI KUTOWA SHUKRANI KWA KAMPUNI HIYO YA GLOBAL KWA KUTUSHIRIKISHA.

TUMEWATEUWA MABONDIA FRANCIS MIYEYUSHO NA THOMAS MAHALI [SIMBA ASIYEFUGIKA]  ILI WAWEZE  KUPAMBANA NA MABONDIA WA NJE YA TANZANIA KUTOKA KENYA AU UGANDA BADO TUMO KATIKA MAWASILIANO NA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA WA NCHI HIZO MBILI ILI WAWEZE KUTUPATIAN  WAPINZANI WA MABONDIA WETU WA TANZANIA.

NINATOWA WITO KWA WAPENZI WOTE WA NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA KUHUDHURIA KWA WINGI SANA KATIKA UWANJA MKUU WA TAIFA SIKU HIYO YA TAREHE 07-07-2013, KUWEZA KUONA MABONDIA WETU WAKILIWAKILISHA TAIFA LETU ,PIA WAWEZE KUCHANGIA  UJENZI WA MABWENI KWA AJILI YA DADA ZETU

TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA YANAYIJIRI KATIKA MAANDALIZI KADRI YATAKAVYOKUWA YANATOKEA.


                     IMEANDIKWA  NAMI [-


               YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                  RAIS -TPBO-LIMITED

                  +255-713-644974

No comments:

Post a Comment