Tangazo

Pages

Thursday, June 13, 2013

KING CLASS MAWE AENDELEA KUJIFUA PR PHOTO STUDIO YATOA UDHAMINI MDOGO

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akinolewa na Kocha wa mcherzo huo Mohamed Chipota wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi ILala Amana CCM Class anajiandaa na mpambano wake na Patrick  Kavako'Baunsa' wa Morogoro mpambano utakaofanyika june 16 katika ukumbi wa panandi panandi ilala bungoni jumapili hii picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa mchezo wa masumbwi Mohamed chipota kushoto akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo wake utakaofajika jumapili ya juni 16 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni kukabiliana na Patrick  Kavako'Baunsa' wa Morogoro picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 

KAMPUNI ya PR Photo Studio na wamiliki wa mtandao wa http://prhabari.blogspot.com/  chini ya Mwenyekiti wake Spear Patrick wameamua kutoa Udhamini mdogo katika masumbwi kwa kumuwezesha bondia Patrick  Kavako 'Baunsa' wa Morogoro  kumgalamia maradhi pindi afikapo jijini Dar es salaam  siku ya Ijumaa mpaka siku ya mpambano wake jumapili dhidi ya

  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' siku ya jumapili ya june 16 katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Bungoni

Mpambano huo ulioratibiwa na Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  amesema kuwa mpambano huo ambao ni wa raundi nane utakuwa chachu kwa mabondia kureta hamasa ya mchezo wa masumbwi nchini

 kwani tumeweka vijana tofauti tofauti kutoka morogoro na Dar es salaam ambapo itatia hamasa kuendelea kwa mchezo huo hivyo tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kufadhili mchezo wa masumbwi ata kwa udhamini mdogo ili kila eneo la nchi yetu ipate mabondia wacheze mchezo huu

Mpambano huo utakao simamiwa na Kinyogoli Fondition na Shirikisho la masumbwi nchini PST  umerenga kupandisha viwango vya mabondia chipkiz ili wapate michezo mara kwa mara pindi inapotokea

Mbali ya mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi Yohana Robart atapambana na Mussa Sunga na Abuu Mtambwe atamenyana na Kassimu Gamboo

pia kutakuwepo na mapambano mengine ya utangulizi yatakayo usisha mabondia wanawake

 

 
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo , alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

 
No comments:

Post a Comment