Tangazo

Pages

Thursday, December 29, 2011

NGUMI ZA RIDHAA NCHINI WAOMBA WAFADHILI KUJITOKEZA KUCHANGIA

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) limewataka watanzania kuchangia maandalizi ya timu ya Taifa itakayokuwa na kibarua cha kufuzu kucheza michuano ya Olimpiki itakayofanyika Casablanka, Misri Oktoba 15 mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema makampuni mbalimbali wanayoyaomba udhamini huwaambia kuwa hawana sera ya kudhamini mchezo wa ngumi jambo ambalo linawafanya kuwa katika hali ngumu ya kuandaa timu ya Taifa.
"Tunawaomba watanzania kuichangia timu hii ili iweze kupata maandalizi mazuri ya kufuzu, kucheza Olimpiki kwa kuwa ukweli ni kwamba kampuni mbalimbali tunazoziomba udhamini zinatuambia kwamba hazina sera ya kudhamini mchezo huu,"alisema Mashaga.
Alisema wamekuwa wakiandaa timu ya taifa katika mazingira magumu na kwamba wanalishukuru Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kwa kujitolea mara kwa mara katika kuisaidia timu hiyo.
Timu hiyo ya Taifa  inatakiwa kufuzu, kucheza michuano ya Olimpiki kupitia mashindano mbalimbali ya Kimataifa yanayotambulika na Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) kwa mwakani ambapo kwa mara ya mwisho timu ya ngumi ilifuzu michuano hiyo mwaka 2007 kupitia bondia Emmilian Patrick.
mwisho

No comments:

Post a Comment