TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
YAH; KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUFANYIKA KWA
KOZI YA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA
SASA YATAFANYIKA TAREHE 17/11/2011 KIBAHA PWANI
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wamelazimika kusogeza tarehe ya kufanyika kozi ya kimataifa ya walimu 30 wa kufundisha mchezo wa ngumi.Sasa itafanyika kuanzia tarehe
17-25/11/2011 Kibaha Pwani.
Awali kozi hiyo ilikuwa ifanyike kuanzia kuanzia tarehe 12-18/11/2011 Kibaha Pwani.
Sababu ya kusogezwa kwa kozi hiyo,imetokana na mkufunzi mkuu wa kozi hiyo,ambaye ameteuliwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Azzedin Aggoune kutoka Algeria,kuomba kozi hiyo isogezwe mbele kutokana na yeye kupata dharula nchini kwao na kushindwa kufika hapa nchini kama ilivyokuwa imepangwa.
Awali mkufunzi huyo ilikuwa awasili hapa nchini tarehe 11/11/2011,kutokana na dharula iliyompata sasa atawasili hapa nchini tarehe 16/11/2011.
Aidha kwa sasa makocha hao watalazimika kuhudhuria mashindano ya Kova Cup yatakayoanza kufanyika tarehe 14/11/2011 PR Stadium Hotel.zamani Imasco Centre.
Makore Mashaga
KATIBU MKUU BFT.
Mob; 0713588818.
No comments:
Post a Comment