Tangazo

Pages

Monday, September 12, 2011

Klitschko atetea taji lake la WBC KWAKUMTWANGA, TOMASZ ADAMEK





BONDIA Vitali Klitschko ametetea vyema taji lake la uzani wa juu linalotambuliwa na Shirikisho la Masumbwi Ulimwenguni WBC baada ya kumsimisha mpinzani wake,Tomasz Adamek katika raundi ya 10 ya pmbano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana mjini Wroclaw.
.

Kwa mujibu wa Shirika la Habri la Marekani AP,mwamuzi kutoka Italia, Massimo Barrovecchio alisimamaisha pmbano hilo dakika mbili na sekunde 20 ili kumnusuru bondia huyo baada ya kupokea makonde mfululizo kutoka kwa bingwa huyo raia wa Ukrain.

AP iliripoti kuwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 40, Klitschko alikuwa akimzidi mpinzani wake kwa urefu wa inchi sita mpinzani wake jambo ambalo lilimsaidia kumbana Adamek mwenye umri wa miaka 34 katika raundi ya pili,sita na tisa.

Kwa ushindi huo Klitschko amedhihirisha ushindi wake wa mapambano 43-2 yakiwemo 40 aliyoshinda kwa knockout huku Adamek akiendelea kubaki na ushindi wake wa mapambano 44-2.

Kwa matokeo hayao pia yanamfanya Klitschko na mdogo wake Wladimir kutetea ubingwa wao mara tatu katika uzani wa juu katika mashindano yote.

“Nadhani mwamuzi amewafanya maamuzi sahihi . Lakini alipaswa kufanya hivyo mapema ,” alisema Wladimir,ambaye anashikilia mataji ya IBF na “super” WBA sambamba na mataji ya WBO na IBO.

Wladimir alisema kuwa pambano jingine la Klitschko litakuwa ni Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment