Tangazo

Pages

Friday, October 14, 2011

NGUMI KULINDIMA ILALA MBUNGE WAKE KUSHUUDIA




ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.

Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo Aliongeza kuwa katika mapambano hayo mgeni mwalikwa ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye kwa mara ya kwanza atangalia mchezo huo ukipigwa katika jimbo lake

Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwa siliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D Boxing Coach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa

DAVID HAYE ATUNDIKA GLOVE


LONDON, Uingereza
BONDIA David Haye juzi (Juni 13,2011) alitangaza rasmi kustaafu ngumi wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 31, huku akisema kuwa anataka kitu kimoja, kufunga mdomo wake zaidi na hana nafasi ya kupigana na Vitali Klitschko ambaye aliagiza kambi yake kumshawishi
Nyota huyo ametangaza kustaafu kucheza ngumu baada ya Alhamisi kutimiza umri wa miaka 31, katika pambano lake la mwisho alipoteza dhidi ya Wladimir Klitschko.
Baada ya kuingia katika uzito wa juu, Haye alikuwa akitoa maneno ya kuwaudhi wapinzani wake, ikiwa ni pamoja na kuvaa fulana ambayo inapicha inayomwonesha ameshika vichwa vya mabondi wa familia ya Klitschko, Wladimir na Vitali.
Pia alitoa maneno makali kabla ya mechi yake dhidi ya Audley Harrison kwa kusema itakuwa kama ni ubakaji.
Badala ya kutumia nafasi yake hiyo ya kustaafu kuomba radho kwa maneno yake mabaye alisema kuwa anaweza kuchonga zaidi kama atakuja kupigana tena.
Bingwa huyo wa zamani wa WBA alitetea tabia yake ya kutoa maneno makali akisema kuwa ilisaidia kuleta msisimko kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya Wladimir na Nikolai Valuev ambapo tiketi nyingi ziliuzwa na wengi kuangalia kupitia televisheni kwa kulipia.
Alisema kwa kupiti mchezo huyo imesaidia kukusanya fedha.
Alisema amestaafu kwa kufuata ahadi yake kuwa atapigana kwa miaka 10 kisha kustaafu akiwa na miaka 31.
Alipigwa na Wladimir Julai na kusema kuwa bingwa wa WBC, Vitali amepoteza nafasi ya kupigana naye kwa kutokubali alipotoa ofa hiyo.
Haye alisema awali hakutaka kupigana na yeye ila kurudiana na kama kaka yake Wladimir, alipotoa wazo hilo hakuonekana kukubali.

ISSA SEWE AJIFUA KUMKABILI RAMADHANI SHAULI


Kocha mkongwe wa mchezo wa ngumi , Habibu KInyogoli (kulia) akimwelekeza jinsi ya kutupa masubwi bondia Issa Sewe wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam jana Sewe anajiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauli litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Wednesday, October 12, 2011

BONDIA AMIRI KHAN ATAKA KUREJESHA NGUMI WASHINGTON

Khan ataka kurejesha ngumi Washington

WASHINGTON,Marekani

BONDIA raia wa Uingereza Amir Khan, anajiandaa kurejesha masumbwi katika mji mkuu wa Marekani Washington DC atakapopanda ulingoni Desema 10 mwaka huu, kupambana na mpinzani wake mzaliwa wa mji huo, Lamont Peterson.

Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kufanyika katika mji huo, baada ya bingwa wa zamani wa uzani wa juu, Mike Tyson kupigwa na bondia Kevin McBride mwaka 2005.

Pambano hilo pia litakuwa ni la kwanza tangu Khan aongeze ushindi wake wa 26-1 alipomshinda kwa KO, bondia Zab Judah, Julai 23  mwaka huu na kutetea mataji yake ya WBA na IBF.

Bondia huyo alikubali kuzichapa na Peterson mjini Washington, baada ya kufanya ziara mara kadhaa mjini humo, ikiwemo ya Septemba 10 mwaka huu ambapo alikula chakula cha usiku White House dinner.

“Tunataka kurejesha ngumi Washington na ili nadhani litakuwa ni pambano la kwanza kati ya mapambano mengi yatakayofanyika mahali hapa,” alisema  Khan, ambaye atakuwa akitimiza miaka 25 siku mbili kabla ya pambano hilo.

MASUMBWI KULINDIMA ILALA JUMAPILI


Sunday, October 9, 2011

DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI



http://3.bp.blogspot.com/-EjllZT6LNOk/Tkj15jBW8wI/AAAAAAAAEOw/1ZDHd3LqhkQ/s1600/super+d+banner.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-EjllZT6LNOk/Tkj15jBW8wI/AAAAAAAAEOw/1ZDHd3LqhkQ/s1600/super+d+banner.jpg
DVD ZA  SUPER D BOXING COACH KUINGIA SOKONI
DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI KWA AJILI YA MAFUNZO YA MCHEZO HUO HIVI SASA KWA MATAJI YA JUMLA NA REJAREJA PIGA SIMU 0787/0774/0715/0754/0733/0713-406938 AU FIKA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI 0652755838

MKENYA AMSULUBU MTANZANIA BILA HURUMA


Bondia, James Onyango kulia kutoka, Kenya akimsulubu, Abdallah Mohamed , wakati wa mpambano wa kirafiki uliofanyika, ukumbi wa DDC Keko jana, Onyango alisghinda kwa KO raundi ya nne
Bondia, James Onyango kulia kutoka, Kenya akimsulubu, Abdallah Mohamed , wakati wa mpambano wa kirafiki uliofanyika, Onyango alisghinda kwa KO raundi ya nne