Tangazo

Pages

Saturday, October 6, 2018

MABONDIA KUTOKA KWA SUPER D COACH WACHANGIA DAMU KUOKOA MAISHA

Bondia Iddi Mkwela akietoa Damu wakatiwa kampeni ya uchangiaji wa Damu Salama kwa ajili ya kuokowa Maisha  iliyofanyika katika makutano ya mtaa wa Likoma na Agrey Dare Es Salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mdungaji wa sindano kwa ajili ya utoaji wa Damu Rosemary Bulemo kutoka kitengo cha Damu Salama Kanda ya Mashariki akimchoma sindano Bondia Idd Mkwela kwa ajili ya kuchangia Damu uliofanyika katika makutano ya mtaa wa Likoma na Agrey Dar es salaam Picha na  SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kulia akiwa na Bondia Iddi Mkwela mwenye kibagarashia wakiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa Damu ambao wapo katika kikundi cha Upendo Group kilichopo Kariakoo Dar es salaam  Picha na  SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

BAADHI YA MABONDIA wamechangia Damu kwa ajili ya kuokowa maisha mabondia hawo wanaotoka katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM wamejitolea kuchangia Damu kwa jamii kwa kuokoa maisha ya watanzania akizungumza wakati wa uchangiaji huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

Amesema kuwa wameamua kuchangia Damu kwa kuwa wameona jamii nyingi inayo wazunguka ina tatizo la damu kutokana na mambo mengi ya ajali zinazotokea barabarani na wanakuwa na mahitaji mengi yanayousu Damu 

alisisitiza kuwa Super D Boxing Promotion imejizatiti kuitumikia jamii kwa mambo mbalimbali ikiwemo kuchangia Damu pamoja na kujitolea kufanya kazi za kijamii

na ndio maana tumeamua kuja kujitolea Damu kwa mabondia wangu ambao na Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Hussein Shemdowe na Bilali Ngonyani ambao wamejitolea kutoa Damu

nae Bondia machachali Iddi Mkwela aliongeza kwa kusema kuwa ameamua kujitolea Damu ni kwa sababu ameona watu wengi wana mahitaji ya kupatiwa na ukiangalia jamii inayotuzunguka nayo ina maitaji zaidi hivyo nashauli watanzania tuwe na moyo wa kujitolea Damu ili iwe akiba mana na wewe ukipungukiwa siku yake unachukuwa bila galama kwani Damu aiuzwi popote

ni uchangiaji wa hiali kujitolea wewe mimi na yule nawaomba wanamichezo wajitolee kuchangia kwani ni moja ya sadaka zetu hapa Duniani

uchangiaji huo wa Damu ulifanyika katika makutano ya mtaa wa Likoma na Agrey ambapo zaidi ya watu 140 walijitokeza kuchangia na kupatikana lita za kutosha tu kwenye kampeni hiyo

No comments:

Post a Comment