Tangazo

Pages

Tuesday, July 24, 2018

MABONDIA WA KIKE KUZITWANGA SIKU YA NANE NANE DAR LIVE MBAGALA

Mabondia wa kike Maimuna Hashimu kushoto akitunishiana misuli na Happy Daudi mara baada ya kusaini makataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya tarehe nane mwezi wa 8 sikukuu ya nanenane katika ukumbi wa Dar Live uliopo mbagala Dara es salaam wakisindikiza mpambano wa Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' na Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' siku hiyo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

PROMOTA wa ngumi za kulipwa Zahoro Maganga amewasainisha mabondia wa kike Maimuna Hashimu pamoja na Happy Daudi kuzipiga siku ya sikkuu ya nane nae katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam

Maganga amesema kuwa ameamuwa kuwa sapoti wanawake kwa kuwa wanafanya sana mazoezi kwa mda mrefu na wapo wachache katika mchezo uho hivyo ameamuwa kuwachezesha siku hiyo ili kuinua ngumi za wanawake nchini

haidha siku hiyo kutakuwa na mapambano mengi ya kukata na shoka likiwa lile linalo subiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini ni kati ya Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na Abdalla Pazi' Dula Mbabe' watakaozipiga siku hiyo

na Shomari Milundi atazipiga na Ramadhani Migwede  wakati Shabani Kaoneka ataonesheana umwamba na Paul Kamata siku hiyo mbali ya mchezo wa masumbwi kutakuwa na burudani mbalimbali za michezo

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo zilizo tahalishwa na kocha mahiri katika mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  ndani yake pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi zilizopiganwa nchini 

No comments:

Post a Comment