Mabondia Shedrack Ignas kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Ruwanje baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika October 2 katika ukumbi wa white house Bar Kimara Korogwe Picha naSUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Said Chino akitunishiana misuli na Haidar Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Rojas Masamu baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao kesho katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Dar es Salaam SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Manyi Issa kushoto akitunishiana misuri na Mustafa Doto baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumapili katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe Dar es salaam SUPER D BOXING NEWS |
Baadhi ya mabondia makocha na wadau wa mchezo wa masumbwi wakiwa wamesimama kwa ajili ya kufatilia mafunzo hayo
Ofisa Vijana Mstaafu Robert Semkiwa kushoto akisisitiza jambo
Mkurugenzi wa Tasisi isiyo ya kiserekali YOWEDE BW. Edwin Mutayoba akisisitiza jambo wakati wa semina ya ujasiliamali kwa wanamichezo wa mchezo wa ndondi |
Mwenyekiti wa marefarii wa mchezo wa ngumi Tanzania 'TPBC' Ally Bakari 'Champion' akifafanua jambo kwa mabondia |
Na Mwandishi Wetu
BABONDIA mbalimbali wamepima uzito na kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali kabla ya mpambano wao utakaofanyika siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Bar Kimara Korogwe wamepimwa uzito pamoja na Afya zao
akizungumzia mpambano uho kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye pia ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wamepima uzito pamoja na Faya Zao na kupatiwa semina ya ujasiliamali
Aliwataja baadhi ya mabondia waliopima
uzito ni Said Chino atakaezitwanga na haidar Mchanjo uzito wa kg 57 raundi sita wakati Abdallah Ruwanje atavaana na Shedrack Ignas mpambano wa raundi sita la uzito wa kg 63wakati bondia mkongwe kabisa katika mchezo wa masumbwi nchini Mustafa Doto atazipiga na bondia chipkizi Manyi Issa katika uzito wa kg 61 raundi sita
mipambano mingine itawakutanisha mabondia Mohamed Muhunzi atakaepambana na Kassim Ahmad na Hashimu Chisora atazipiga na Rojas Masam uzito wa kg 61 na Julias Jackson atapambana na Emilio Norfat mpambano wa raund 4 uzito wa kg 61 na Ellsame Mbwambo atazipiga na Emanuel Kisawani mpambano wa raundi 4 uzito wa kg 61
mbali ya siku ya leo kesho tena
kutakuwa na elimu ya ujasiliamali kwa vijana wa mchezo wa masumbwi pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujikwamuwa na uchumi
Mgeni rasmi katika mpambano uho atakuwa
Humphrey Polepole Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
Katika Mchezo huo kutakua na Uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi
No comments:
Post a Comment