TAREHE 27/12/2012
Shirilisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis
Cheka.
Katika
barua yake aliyomtumia Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa
kamati ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema "Tunachukua
fursa hii kukutakia maisha na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza
kuishi kama bingwa". Cheka atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi
sita kufikia mwezi wa 6 mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na mengi
awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho.
Aidha IBF
inampongeza bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu wake na ushindani
mzuri katika pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
katika jiji la Arusha tarehe 26 Desemba, 2012.
Imetolewa
na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais
IBF/USBA Afrka, Ghuba ya Uajemi an
Mashariki ya Kati
CHIOTCHA
AONJA MACHUNGU YA CHEKA
Bondia
kutoka Jamhuri ya watu wa Malawi Chiotcha Chimwemwe alionja machungu ya
Mtanzania Francis Cheka katika mpambano wao uliopewa jina na “Vita vya Ziwa
Nyasa” tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day jijini Arusha.
Ulikuwa ni mpambano
wa mwaka ambao bondia Francis Cheka nusura aupoteze katika raundi ya pili
wakati konde zito la kushoto la kapteni Usu kutoka katika jeshi la jamhuri ya
watu wa Malawi, Chiotcha lilipompeleka chini na kuinuka kwa msaaada wa kamba za
ulingo.
Konde hilo
zito lilifungua mpasuko mkubwa katika paji la Cheka na hivyo kuleta wasiwasi
kwa mashabiki zaidi ya elfu 10 waliofurika katika uwanja wa Sheikh Amri Abed
kumshughudia Cheka akipambana kiume kwelikweli.
Raundi ya
kwanza mpaka ya nne Chiotcha alikuwa anamiliki mpambano huo na makonde mazito
ya mkono wake wa kushoto kwani anatumia staili ya South Paw inayomlazimu kutanguliza
mbele mguu wa kulia.
Ni katika
raundi ya sita ambako Cheka aliweza kubadilisha mwelekeo wa mpambano kwa kuanza
kumwadhibu Chiotcha na makonde mazito ya kombinasheni yaliyomfanya Mmalawi huyo
kumkumbatia bila mafanikio Mtanzania huyo asiyepigika.
Cheka
aliwanyanyua mashabiki waliojaa uwanjani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa jiji
la Arusha, Mh. Gaudence Lyimo alipompiga bila huruma Chiotcha na kumlazimu
refarii wa kimataifa wa mpambano huo Nemes Kavishe wa Tanzania kumwonya kutomshika
Cheka kama vile anapigana mieleka.,
Juhudi za
Chiotcha kujisalimisha kwa kumkumbatia Cheka hazikuzaa matunda kwani aliendelea
kupewa mkong’oto na mwana huyo wa Kitanzania aliyejizolea sifa kemkem kwa kuwapiga
wapinzani wake.
Mashabiki
wengi walinyanyuka katika viti vyao katika raundi ya 12 ya lala salama wakati
Cheka alipodhihirisha kweli ni bondia asiyepigika kwa kumpiga makonde mazito
kichwani Chiotcha na kumfanya apepesuke kila mara.
Katika
mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Green Hills (T) Investment ya jijini
Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na bingwa wa zamani wa taifa Andrew George,
mabondia wa mapambano ya utanguliizi walikuwa wa ngumi za ridhaa kutoka katika
jiji la Arusha.
Mpambano huo
ulisimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi akisaidiwa na Kamishna wa TPBC kutoka Jiji la
Arusha bw. Roman Chuwa.
Refarii
alikuwa Nemes Kavishe kutoka Tanzania wakati majaji walikuwa: Daudi Chikwanje
kutoka Malawi, Boniface Wambura kutoka Tanzania na Galous Ligongo kutoka
Tanzania.
Imetolewa na
Uongozi, TPBC
No comments:
Post a Comment