Tangazo

Pages

Tuesday, February 7, 2012

Rashidi MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA Februar 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR




BONDIA wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla 'Snek man' amesema kukutana ulingoni mara kwa mara na bondia Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' hawachezei njaa isipokuwa ni mapenzi ya ngumi aliyokuwa nayo.

Matumla na Maneno wanakutana ulingoni kwa mara ya tano sasa ambapo baadhi ya wadau wamekuwa wakihisi labda mabondia hao hupigana kwa sababu ya kutafuta fedha.

Akizungumza kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Matumla alisema yeye binafsi bado anauwezo wa kupigana katika mchezo huo na kama angetaka kustaafu angeweza kufanya hivyo ila bado anayo nafasi ya kufanya vizuri katika mapambano yake.

Alisema pambano lake dhidi ya Maneno litakalopigwa Februari 25 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba litakuwa ni pambano lake la tano kukutana na bondia huyo.

"Mimi na Maneno tumeshakutana mara nne ulingoni hadi sasa na hili litakuwa ni pambano letu la tano kupigana,"alisema Matumla na kuongeza kuwa.

"Katika mapambano hayo nimemshinda Maneno mapambano mawili, amenipiga pambano moja na tumetoka sare pambano moja lakini kama itawezekana nitamtwanga katika pambano lijalo,"alisema Matumla.

Alisema kwa sasa anajifua chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambaye ameingia naye mkataba wa kumnoa na anainami atafanikiwa kumtwanga Maneno katika mchezo huo.

Pambano hilo la Februari 25 litakuwa ni pambano la marudiano kwa mabondia hao baada ya kutoka sare katika pambano la kwanza lililofanyika katika ukumbi wa Henken Mtoni Desemba 25 mwaka jana.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

No comments:

Post a Comment