Na Mwandishi wetu
Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira wa ( morogoro ) katika pambano lake litakalo fanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 uliopo mwenge jeshini mpambano huo ambao umewekwa kwa ajili ya kupandisha viwango mabondia mbalimbali litakuwa ni sehumu moja ya kuwapongeza mabondia
waliofanya vizuri nje ya nchi na kurudi na mikanda mikubwa nchini miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili mabondia hawo wameleta mikanda hiyo nchini ndani ya mwezi mmoja tu
Makubi ametamba kumsambalatisha bila huruma yoyote ile Abdalah wa morogoro kwani ushindi wake ndio utakao msafishia njia ya kwenda juu zaidi katika mapambano ya ngumi anajua kuwa ngumi sio mchezo raisi kama ilivyo kwa michezo mingine
nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anaemnowa na kumtafutia mambambano kwa ajili ya kumpandisha Daraja bondia huyo amesema kwa sasa makubi kila pambano lake kwake ni fainal kwani hapa kazi tu No Pain No Gain tutaakikisha tunashinda kila pambano na mpaka atakuwa bingwa wa mabingwa nchini na Duniani alisema Kocha Super d
Pages
▼
Friday, September 27, 2019
BONDIA JUMA CHOKI SASA AWAZIA UBINGWA WA TAIFA BAADA YA KUWA KING OF THE RING
NA MWANDISHI WETU
BONDIA Juma Choki Baada ya kumgalagaza bila ya huruma Emanuel Mwakyembe na kuchukua ubingwa wa King Of The Ring 2019 katika uzito wa KG 58 amesema ato bweteka kwa kuwachua ubingwa huo
ambapo alipewa zawadi ya pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano amesisitiza ato bweteka kwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ata hivyo ameomba kuwa andaliwe ubingwa wa taifa ndio matarajio yake kwa sasa akichukuwa ubingwa wa taifa kisha ataenda juu kuchukuwa ubingwa wa Afrika arafu ubingwa wa Dunia
Bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuchukuwa mikanda nje ya nchi na kuletea sifa Tanzania
Akizungumza kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa choki ni bondia mzuri na malengo yake ni kufika mbali na kweli atafika anapo pataka kwani kwenye nia pana njia
ikumbukwe kuwa mimi ndio nimewatoa mabondia mabingwa wa dunia ambao wamepita katika mikono yangu kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Sunday Kiwale Ibrahimu makubi ambaye kwa sasa yupo mazoezini akijiandaa na mpambano wake na abdallah kingolwira wa morogoro pambano litakalofanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 mwenge pale jeshini
hivyo nina uwakika na mabondia wangu wote ninaowafundisha na siku zoto sinaga kazi mbovu
NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE
Mabondia wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia wenzao .
Aliwataja miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote bingwa na wameletea taifa heshima kubwa wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.
" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.
Aliongeza kuwa pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano la funga mwaka.
" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa kipindi cha hivi karibuni itawekwa " Alisema Semunyu.
Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali kwa wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.
Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe (Dsm) vs alli hamisi (morogoro )
Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira ( morogoro )Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) )Hashimu msungo vs Epson john Lewis Salumu omari vs ramadhani chicho
Aliongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na mabondia wengine kutafuta nafasi ya kutaka kushiriki Desemba lakini wengine nao wanataka kushiriki kuonesha furaha ya ushindi huo
Saturday, September 14, 2019
MABONDIA JUMA CHOKI NA EMANUEL MWAKYEMBE WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO SEPTEMBA 15 MASAKI
|
Tuesday, September 10, 2019
JUMA CHOKI AJIFUA KUMKABIRI MWAKYEMBE SEPTEMBA 15
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kamba ya Super D coach Shule ya Uhuru Dar es salaam Jana |
Bondia Alex Kachelewa kushoto akitupiana makonde na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D coach shule ya Uhuru |
Na Mwandishi Wetu
Bondia Juma Choki anaye jiandaa na mbambano wake dhidi ya Emanuela Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket Clab uliopo Masaki jijini Dar es es salaam amejinasibu kumtwanga bondia huyo na kuchukuwa ubingwa wa king of The Ring
akijinasibu bondia huyo alivyotembelewa kambini kwake kwa Super D Coach iliyopo shule ya Uhuru Jijini Dar es salaam
Amesema kuwa mwakembe ana uwezo wa kukanyaga moto wake ata siku moja huko alikutana na viande sasa kaja kwenye kazi kazi hapo ndipo pa kuoneshana uwezo kama anavyosemaga kocha Super D Kazi Kazi No Pain No Gain yani siku hiyo patachimbika hivyo mwakyembe ajipange sana kwana mazoezi ninayofanya na mbinu ninazofundishwa sio za kitoto hatari tupu
Nae kocha wa bondia huyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema hii ni vita kubwa sana kwa kuwa kocha wa mwakyembe Edward Lwiyakwipya wamesoma nae pamoja katika ngazi kubwa ya kozi ya kimataifa hata hivyo mimi nina mbinu nyingi zaidi yake ata hivyo nita akikisha napata ushindi usiokuwa wa kuwachosha majaji hivyo matumaini yangu ni kumpiga k,o mbaya zaidi
ikumbukwe kuwa mabondia wote wenye viwango vya juu nchini wanatoka kwangu ukiangalia mabondia wote wakubwa wanatoka kwangu na wana viwango vya kimataifa hivyo najivunia kwa hilo ukiangalia mabondia wanaotoka kwangu akuna ata mchovyu mmoja alijinasibu Super D
Aliongeza kwa kusema mikono yake wamepita mabondia wengi sana akiwemo Sanday Kiwale, Idd Mkwera Vicent Mbilinyi Ibrahimu Class' King Class Mawe' Shomali Milundi Shabani Kaoneka na mabondia mbalimbali nchini wote wamepita katika mikono yangu kwa njia moja au nyingine hapa ndio No Pain No Gain kazi kazi hivyo wapenzi wa ngumi muje kwa wingi kuangalia kazi hii ambayo aita muacha mtu salama