Pages
▼
Sunday, November 30, 2014
BABU WA MIAKA 63 AMPIGA KO RAUNDI YA PILI 'DOGO' WA MIAKA 33
KAMA ingekuwa sinema ya Hollywood, ingekuwa bomba sana.
Lakini Mickey Rourke hakuwa anaigiza jana wakati alipopanda ulingoni baada ya miaka 20 ya kuachana na ndiondi na kumpa mtu kichapo.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 alizipiga na Elliot Seymour, mwenye umri wa miaka 33, katika pambano la raundi tano Moscow, Urusi. Rourke alihitaji randi mbili tu kumsimamisha mpinzani wake ambaye alianguka chini baada ya kupewa 'mkono mkali' wa mtu mzima huyo.
Baada ya mapambano 30 katika ngumi za Ridhaa, miaka ya 1960 hadi 70, ambayo alipoteza matatu tu, Rourke alihamia kwenye kucheza filamu Hollywood, kabla ya kurejea kwenye mchezo kama bondia wa kulipwa miaka ya 90, ambayo ilimsababisha athari usoni mwake na kulazimika kufanyiwa upasuaji uliobadilisha mwonekano wa sura yake. Alishinda pambano moja tu kati ya tisa ya kulipwa.
Nyota wa Hollywood, Mickey Rourke akiinuliwa mkono kutangazwa mshindi baada ya kumkalisha Elliot Seymour raundi ya pili
TYSON AMSHINDA CHISORA, SASA KUMVAA KLITSCHKO
Bondia Tyson Fury (kulia) akimchapa konde la uppercut mpinzani wake Dereck Chisora katika pambano la uzito wa juu usiku wa jana ukumbi wa ExCel, Docklands mjini London. Fury alishinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10 na sasa anaweza kupambana na bingwa wa dunia, Wladimir Klitschko mwakani.
TOTO LA CHRIS EUBANK LACHAPWA NA MZUNGU
Bondia Billy Joe Saunders (kulia) akipambana na Chris Eubank Junior kushoto usiku wa jana ukumbi wa ExCeL mjini London, katika pambano la uzito wa Middler. Saunders alishinda kwa pointi na kutetea mataji yake ya Uingereza, Jumuiya ya Madola na Ulaya- na sasa amepewa nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia wa WBO mwakani.
Chris Eubank (katikati) akimpongeza Saunders kwa ushindi dhidi ya mwanawe jana
Friday, November 28, 2014
Saturday, November 22, 2014
BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA ALIVYOKUTANA NA WATU MAARUFU MACAU CHINA
KUTOKA KULIA: Emmanuel Mlundwa ; Fadhili Majiha NA MTANGAZAJI MAARUFU WA MASUMBWI DUNIANI Michael Buffuer AMBAYE HUSEMA :" AND MILLIONS OF VIEWERS AROUND THE WORLD, GET READY TO RUMBLE "
FROM LEFT: Emmanuel Mlundwa; Fadhili Majiha AND Freddie Roach Official THE TRAINER OF Manny Pacquiao . 22/11/2014 AT THE CAPRI ARENA, MACAU
Fadhili Majiha [LEFT] WITH Roy Jones Jr AT THE CAPRI ARENA, MACAU 22/11/2014
Friday, November 21, 2014
BONDIA ZUMBA KUKWE KUZIPIGA NA SWEET KALULU
Bondia wa
ngumi za kulipwa nchini mwenye machachali mengi na ngumi nzito awapo
ulingoni Zumba Kukwe “chenji dola” anatarajia kupanda ulingoni alhamis ya
tarehe 27/11/2014 kuzipiga na bondia mkongwe Sweet kalulu katika ukumbi wa kontena uliopo kibaha maili moja,
Watacheza pambano la raundi nane, lisilo la ubingwa ila mshindi kati ya sweet
kalulu na zumba kukwe atacheza na mshindi kati ya Thomas Mashali na dula mbabe
katika pambano la ubingwa, mashali na dula wao wanacheza decemba.
Akilizunguzia
pambano hilo kwa wanahabari kiongozi wa ngumi za kulipwa na mratibu wa pambano
hilo alisema “pambano la Zumba kukwe na sweet kalulu maandalizi yanakwenda
vema chini ya udhamini wa George Nyasulu
aliependekeza mchezo upigwe kibaha maili moja alipotokea zumba kukwe na kutanua
wigo wa masumbwi nchini ,ngumi ziwe zinachezwa kila kona ya nchi sio kila siku
mabondia kucheza mjini dar e salaam tu, watu
wa mkoa wa pwani nao wapate nafasi
ya kuwaona vijana wao wanaotikisa mjini kwani
kibaha kuna mabondia wengi wazuri na wakali ambao hawajawahi cheza kwao , hivyo
katika mapambano ya utangulizi kutakuwepo na mabondia wote wakali wa mkoa wa
pwani wakicheza na wenzao toka sehemu mbalimbali za jiji kama vile Mustafa doto
atazipiga na ramadhan max, huku shadrack ignas akioneshana kazi na fredy masinde,nae dogo janja Issa omar
nampepeche atazipiga na Rajabu miafro na mapambano mengine mengi ya utangulizi .kiingilio
kimepangwa kuwekwa kidogo ili watu wengi wapate kuja shuhudia pambano hilo la
aina yake ambalo si la kukosa
BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA KUMSINDIKIZA MANNY PAQUAIO NOVEMBA 22 MACAO CHINA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Fadhili majiha kwa mara ya kwanza ataiwakilisha nchi ya
tanzania akicheza katika mpambano wa utangulizi wa bondia mkubwa duniani
Manny Paquaio na Chris Algieri mpam
bano utakaofanyika
Cotai Arena, Venetian Resort, Macao, Macao S.A.R., China mpambano ambao bonia mtanzania Fadhili Majiha atavaana na Jerwin Ancajas kutoka Philippines mpambano utakaokuwa wa raundi 8
mch
ezo uliopowa hadhi ya nyota mbili ambapo watanzania wote wanapaswa
kumuombea duwa bondia nambari moja kwa ubora nchini tanzani kwa ajili ya
kutuwakilisha katika mpambano uho mkubwa wa kimataifa ambapo zaidi ya
watu wengi duniani watakuwa wakiangalia mojakwa moja kupitia luninga zao
Majiha ambaye hivi karibuni ametokea nchini Bangkok, Thailand alipocheza mpambano wake wa mwisho wa raundi 12 na kupoteza kwa pointi amewakikishia wa tanzania kuwa bado yupo fiti na atafanya maajabu siku hiyo kwa kumtwanga MPhilippines huyo ambaye atakutana nae siku hiyo |
Monday, November 17, 2014
Laila Ali 'She Bee Stingin'' BONDIA PEKEE WA KIKE ALIYECHUKUA KIWANGO CHA JUU CHA FEDHA KATIKA WANAMASUMBWI
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao |
Kwa sasa unakadiriwa pia utajiri wake
unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni kumi ambazo ni zaidi ya
fedha za kitanzania bilioni 16, ambazo ambazo amezitengeneza kutoka
katika mchezo wa masumbwi duniani,
Matangazo ya bihashara, pamoja na kazi ya uwanamitindo


Ambapo mwaka 2002 alitwaa ubingwa wa super middleweight 17,8,2002 kwa kumtwanga K,O raundi ya pili bondia Suzette Taylor na kutangazwa kuwa bingwa wa Dunia unaotambuliwa na chama cha kimataifa 'IBA'

Pamoja na uwezo huo, Wapo baadhi ya
mabondia wa kike kama Vonda Ward, Leatitia, Robinson na Ann Wolfe
wamekuwa wakilalamika kuwa Leila anawakwepa kwa kupangiwa vibonde na
kuhofia kupigwa.
Licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo
wa masumbwi, mitindo na matangazo ya biashara kwenye runinga lakini mara
kadhaa amekua akialikwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kwa ajili
ya vipindi hali inayomfanya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha
Baadhi ya vipindi hivyo maarufu ni
pamoja na agaeorgr Lpez, Dancing with the Stars, American
Gladiators,Celebrity Family. The Early Show
Katika historia ya maisha yake ya
ndoa ,leila amesha olewa mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa
na Johnny Mcclain Agost 27,2000,ambaye walikutana kwenye sharehe ya
kuzaliwa baba yake mzazi Mohamed Ali wakati anatimiza umri wa miaka 57.
Kabla ya kuoanaMacClain ndiye
aliyekuwa promota wake katika michezo ya ngumi za kulipwa jambo ambalo
lilimsaidia kufanya vizuri katika mapambano yake yote ambayo ajapigwa
wala kutoa droo ata mpambano mmoja akiwa na alama won 24 (KO 21)
+
lost 0 (KO 0)
+
drawn 0
=
24
Baada ya kuoana mwaka 2000 walikuja
kuhachana mwaka 2005. mwaka 2007, leila alifunga ndoa na Curtis Conway ,
ikiwa ni ndoa yake ya pili . wadadisi wa mambo ya kimapenzi wanaeleza
kuwa kilichomfanya kuolewa tena ni kutokana na kuwa na mvuto wa
kimapenzi alionao mwana dada huyo maili awapo ulingoni,
Leila amefanikiwa kupata watoto
watatu akiwa na McClain ambao ni Leilani,Cameron na Kelton. Baada ya
kuolewa tena alipata watoto wawili ambao ni Curtis Muhame Conway
Aliyezaliwa mwaka 2008 na Sydney mwaka 2011
Kwa sasa leila amestafu kucheza mchezo wa masumbwi tangu acheze mchezo wake wa mwisho Tareha 3 -2-2007 na Gwendolyn O'Neil na kufanikiwa kumpiga kwa K,O raundi ya kwanza na kutangazwa kuwa bingwa wa mikata miwili ya WBC female super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
Ingawa kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kutangaza vipindi mbalimbali kwenye television pamoja na mitindo
Moja ya mambo ambayo yalishangaza
ulimwengu katika fani ya mitindo mwaka 2012 akiwa na mimba ya miezi 9,
aliweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya mavadhi aliweza kuonesha
umahiri wake kwenye jukwaa kwa kupita akiwa kwenye tamasha la mavazi
lililofanyika jijini London Nchini Uingereza Novemba 20, 2012
Amestaafu akiwa na rekodi ya kutopigwa ata mchezo mmoja ambapo alicheza michezo 24 alishinda kwa KO 21 ambapo mabondia watatu pekee ndio aliwashinda kwa point
huyo ndio leila Muhamed Ali
kwa mahitaji ya DVD ZAKE KWA AJILI YA KUONA MAPAMBANO YAKE MBALIMBALI LIVE TUWASILIANE KUPITIA
![]() |
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao |
Thursday, November 13, 2014
BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI FRENDS CORNER
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG |
Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana
na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas
katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends
corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
Promota Kassim Texas
katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na SUPER D BLOGMonday, November 10, 2014
MABONDIA IBRAHIMU TAMBA NA JULIUS KISARAWE WANYAKUWA MIKANDA YA TPBO
Bondia Mrisho Adam kushoto akipambana
na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita Adam alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Mrisho Adam kulia akipambana na Mustafa Dotto
wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Adam
alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Karim Ramadhani Kushoto
akipambana na Stevin Kobelo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni
mwa wiki iliyopita mchazo huo ulimalizika kwa droo picha na SUPER D BLOG
Bondia Hassani Kiwale kushoto
akipambana na Julius Kisarawe wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa
wa chama cha TPBO Kisarawe aluishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Maisha Samson kushoto
akipambana na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni
mwa wili iliyopita Tamba alishinda kwa K,O ya raundi ya Pili na
kunyakuwa ubingwa Picha na SUPER D BLOG
Refarii Sako Mtlya akimnyoosha mkono
juu bondia Ibrahimu Tamba baada ya kumgalagaza Maisha Samsoni kwa K,O ya
raundi ya pili katika mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita Picha na SUPER D BLOG
Friday, November 7, 2014
MABONDIA SAMSON MAISHA NA IBRAHIMU TAMBA WATAMBIANA KUZIDUNDA JUMAPILI NOVEMBA 9 MANYARA PARK MANZESE
Bondia Maisha Samson kushoto wakitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Bondia Maisha Samson kushoto wakitunisha misuli na
Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika
jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na
SUPER D BLOG
Samson Maisha
Ibrahimu Tamba
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar kushoto na Samson Maisha wa Kyela
Mbeya wakinyoshwa mikono juu na mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame wakati wa utambulisho wa mpambano wao
utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park
Tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar na Samson Maisha wa Kyela
Mbeya wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao
utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park
Tandale CCM katikati ni mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame Picha na SUPER D BLOG
NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela
Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa
TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika
ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam
mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na
Moro Best mpambano wa raundi kumi pia
mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo
tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima
aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na
mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na
Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Thursday, November 6, 2014
NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela amewasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa TPBO na Ibrahimu Tamba mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam
mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na
Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima
aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Tuesday, November 4, 2014
BONDIA IDDI PIALALI AIBEBA KIWANGWA BAGAMOYO KWA KUNYAKUWA UBINGWA WA KANDA YA MASHARIKI
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG |
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG |
Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Pialali
Bondia Iddi Pialali |
Bondia Hashimu Zuber kushoto
akipambana na Ally Mahiyo wakati wa mpambano wao uliofanyika kiwangwa
bagamoyo mkowa wa pwani Zuber alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia mchezo huo uliopigwa siku ya jumatatu kiwangwa bagamoyo mkoa wa pwani
Bondia Ally Bugingo kushoto akimtupia konde Twalibu Tuwa wakati wa mpambano wao Bugingo alishinda kwa point
Picha na SUPER D BLOG
Said Yazidu akiongea na mashabiki wakati wa mpambano huo
BAADHI YA WATU AMBAO WALIKOSA KUINGIA UKUMBINI KWA KUTOKUWA NA PESA WAKIPIGA CHAPO KWENYE DIRISHA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki hii aliwainuwa mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O ya raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi
mpambano huo uliofanyika siku ya jumatatu ulikuwa na shamlashamla nyingi tangia mwanzoni mwa mchezo huo ambapo watu walifulika kuona ndonga zikipigwa Kiwangwa
mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku
uku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano
kabla ya mpambano huo kulikuwa na mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa pointi Twalibu Tuwa
mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewahaidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki hii aliwainuwa mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O ya raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi
mpambano huo uliofanyika siku ya jumatatu ulikuwa na shamlashamla nyingi tangia mwanzoni mwa mchezo huo ambapo watu walifulika kuona ndonga zikipigwa Kiwangwa
mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku
uku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano
kabla ya mpambano huo kulikuwa na mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa pointi Twalibu Tuwa
mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewahaidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini