Tangazo

Pages

Wednesday, June 15, 2016

MABONDIA GALILE NA MAPAMBANO KUMALIZA UBISHA JULAY 24 MUSOMA BAR

Mdau wa masumbwi nchini Jumanne Mbwembwe akiwainua mikono juu mabondia Imani Mapambano kushoto na Seleman Galile kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Iani Mapambano kushoto na Selemani Galile wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bara tasndika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Imani Mapambano kushoto akitunishiana misuli na Selemani Galile baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julay 24 katika ukumbi wa musoma bar tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Imani Mapambano na Selemani Galile wamesaini mkataba wa kuzipiga Julay 24 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika Dar es salaam

akizungumza baaya kusainishwa kwa mabondia hawo mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 
Amesema amewasainisha mabondia hawo baada ya kutambiana mara kwa mara kadri wakutanapo
hivyo 
nimeamua wapambane julay 24 katika ukumbi wa musoma bar ili kumaliza ubisha wao 
mpambano uho utakuwa wa ubingwa wa Taifa utakaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'Ustadhi' 
Aliongeza kwa kusema kuwa mipambano mingine ya utangulizi watatangaza kadri watakavyo ingia mikataba na mabondia mbali mbali  

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Monday, June 13, 2016

MABONDIA MFAUME MFAUME NA JONAS SEGU SASA KUPAMBANA AGOST 21 TAIFA

Mabondia Mfaume Mfaume kushoto na Jonas segu wakitnishiana misuli baada ya kusaini kuzipiga agost 21 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS



 Mabondia Mfaume Mfaume kushoto akitambiana na Jonas Segu baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Agost 21 katika uwanja wa Taifa katikati ni Promota Dotto Texas Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Mfaume Mfaume kushoto akitunishiana misuli na Jonas Segu baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Agost 21 katika uwanja wa Taifa katikati ni Promota Dotto Texas Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA IBRAHIMU TAMBA NA HUSSEIN ITABA WASAINI KUZIPIGA JULAY 16 MAGOMENI MAPIPA

Mabondia Hussein Itaba kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julay 16 katika ukumbi wa traveltain uliopo magomeni mpipa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Hussein Itaba kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julay 16 katika ukumbi wa traveltain uliopo magomeni mpipa katikati ni Promota wa mpambano uho Dotto Texas Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Tamba kulia akitia saini ya kuzipiga na Hussei Itaba kushoto anaeshudia katikati ni promota wa pambano huo Dotto Texas mpambano utafanyika katika ukumbi wa traveltain uliopo magomeni mpipa  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Hussein Itaba kushoto akitia saini ya kuzipiga na Ibrahimu Tamba kulia anaeshudia katikati ni promota wa pambano huo Dotto Texas mpambano utafanyika katika ukumbi wa traveltain uliopo magomeni mpipa  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Tamba na Hussein Itaba wametia saini ya kuzipiga siku ya julay 16 katika ukumbi wa travertain Magomeni
akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo promota wa mpambano huo Dotto Tesax amesema ameamua kuwakutanisha mabondia hawo ambao ni mahasimu katika kitongoji cha manzese kutaka kujua ni nani zaidi kati yao

mabondia hawo wamekuwa wikitambiana kila kona wanazopita sasa katika kutaka kujua nani zaidi nimeambua kuwandalia mpambano uho ambao utafanyika siku ya julay 16 katika kumbi wa Traveltain magomeni
hivyo napenda kuwambia mashabiki wa mchezo wa masumbwi kujitokeza kwa wngi siku hiyo ambapo kutakuwa na mapambano mengine ya utangalizi ambayo tutawatangazia kadri muda utakapo wadiwa
baada ya kukutanishwa kwa mara ya kwanza mabondia hawo kila mmoja alikuwa na lake la kusema kwa ajili ya kutamba bondia Itaba amesema anashukuru sana kukutanishwa na Tamba kwa kuwa alikuwa ana usongo nae kwa mda mrefu
nae Tamba alijibu mapigo kwa kusema kuwa yeye awezi kupigwa na bondia mgeni katika anga za masumbwi kwa kuwa mpaka sasa ana mechi chache sana katika gem hii hivyo sitarajii kupoteza mchezo wangu kwake nawaomba mashabiki zangu waje kwa wingi waone  ninavyo mgalagaza Itaba bila huruma na sito jari chochoto wakati nipo ulingioni kwani mikono yangu itaongea wakati nipo uringoni 

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Tuesday, June 7, 2016

MWALIMU NYERERE ALIPOMGOMEA MUHAMMAD ALI


•Hii ilikuwa ni Jumamosi tarehe 02-Feb-1980 katika uwanja wa ndege wa Dar-es-Salaam (ambao hivi sasa ni Terminal 1) siku bondia Muhammad Ali alipowasili Tanzania.
•Katika kilele cha vita baridi (cold war), Muhammad Ali alitumwa na rais wa Marekani Jimmy Carter kuja kuishawishi Tanzania isusie mashindano ya Olympic Games ambayo mwaka huo wa 1980 yalikuwa yanafanyika Urusi (USSR) Moscow kutokana na kitendo cha serikali ya ki-soviet kuivamia kijeshi nchi ya Afghanistan mwaka 1979.
•Muhammad Ali, ambaye kabla ya kujiunga na dini ya Black Muslim mwaka 1964 alikuwa anaitwa Cassius Clay, alitumwa kuzishawishi nchi 5 za kiafrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Nigeria, Liberia na Senegal.
•Utamu wa ziara ya Muhammad Ali uliishia uwanja wa ndege ambapo alipokelewa na watu nyomi wakiongozwa na aliyekuwa waziri wa utamaduni Chediel Mgonja. Labda pia na Kilimanjaro Hotel (hivi sasa Hyatt Regen 

alipokaa kwenye ziara hiyo ya siku 3.
•Pamoja na umaarufu wake wa kimichezo na ushawishi mkubwa wa ubalozi wa Marekani, juhudi zake za kukutana na Mwalimu Nyerere zilishindikana kabisa. Inasemekana Mwalimu Nyerere alikasirika na hakutaka kukutana na Muhammad Ali kwa vile aliona Muhammad hakuwa na ngazi ya kidiplomasia ya kuweza kukutana naye.
•Baada ya hapo, “The Greatest” alienda nchi nyingine 4 ambapo Nigeria pia hakupokewa na rais Alhaj Shehu Shagari. Alipokelewa na marais kwenye nchi 3 za Kenya (Daniel arap Moi), Senegal (Leopold Sedar Senghor) na Liberia (William R. Tolbert, Jr). Nchini Senegal alielezwa kwamba nchi ina sera ya kutochanganya mambo ya michezo na siasa. Alifanikiwa kwenye nchi 2 tu za Kenya na Liberia. Ila baadaye Liberia ilibadili msimamo (kabla ya mashindano) baada ya kupinduliwa na kuuwawa kwa rais William R. Tolbert, Jr (Apr-1980). Uongozi wa kijeshi ulioingia madarakani (chini ya Samuel Doe) ukaipeleka timu Moscow lakini baadaye wakaiondoa baada ya sherehe za ufunguzi. Ziara ya Muhammad Ali haikuwa na mafanikio sana kwa vile kama angefanikiwa kuishawishi Tanzania, nchi nyingine nyingi za Afrika zingeweza kubadili msimamo.
•Timu ya Tanzania ilienda Moscow, Urusi kushiriki mashindano na kurudi na medali 2 kutoka kwa wanariadha Filbert Bayi na Suleiman Nyambui (Silver Medals). Hii ndio michuano pekee ya Olympic ambayo Tanzania iliwahi kupata medali. Bila shaka kama nchi nyingine zisingegoma, isingekuwa rahisi Tanzania kupata medali hata moja.
•Lakini kisa kikuu cha mwalimu Nyerere kuwakomalia wamarekani kinatokana na tukio la mwaka 1976 kwenye Olympic Games zilizofanyika Montreal, Canada. Nchi za kiafrika mwaka huo, zikiongozwa na Tanzania, zilisusia mashindano hayo kutokana na kitendo cha timu ya New Zealand kushiriki mashindano hayo. Nchi za Afrika zikiongozwa na Tanzania ziliomba IOC (International Olympic Committee) isiiruhusu New Zealand kushiriki mashindano hayo kutokana na timu yake ya Rugby mwanzoni mwa mwaka 1976 kuzuru Afrika Kusini na kucheza na timu ya Afrika ya Kusini kitendo ambacho kilionekana ni kinyume na maazimio ya kuitenga Afrika ya Kusini kijamii na kiuchumi kutokana na sera za ubaguzi wa rangi (apartheid). Kutokana na ombi hilo kukataliwa ,nchi nyingi za Afrika zilisusia mashindano hayo ya mwaka huo. Nchi nyingine kama Marekani ziliendelea kushiriki bila kuziunga mkono nchi hizo za Afrika bila kujua ambacho kitatokea baadaye miaka mi-4.

MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA WATAKA MALEZI BORA YA MCHEZO UHO

 Mdau  wa mchezo wa ngumi nchini Chaurembo Palasa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini   kushoto ni Chuku Dusso Ally Bakari na Yassin Abdallah Picha na SUPER BOXING NEWS           
 BAADHI YA WADAU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANDO WA KUNUSURU MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA MWENENDO WAKE MZIMA KUTOKA KULIA WALIO SIMAMA NI sHOMARI kIMBAU,SHABANI KAONEKA,CHUKU DUSO Mkali Kaizum CHAUREMBO PALAS NA WALIOKAA KUTOKA KUSHOTO NI FIDEL HYNES  ALLY BAKARI NA RATIBU WA MKUTANO UHO SADICK KINYOGOLI
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Yasin Abdallah katikati akiongea katika mkutano wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini kushoto ni Chuku Duso na kulia ni Chaulembo Palasa Picha na SUPER BOXING NEWS
Katika miaka ya hivi karibuni takwimu zinaonesha kuwa masumbwi ndio mchezo wenye kuingiza pesa nyingi kuliko mchezo wowote duniani, ambapo kwa hivi sasa kinara wa utajiri kupitia mchezo huo ni bondia Floyd Mayweather.
Mkali huyo anafuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia wanaoshikilia nafasi mbili za juu za utajiri michezoni, huku  michezo mingine ikifuata.

lakini kwa hapa kwetu Tanzania kumekuwa na kilio cha kawaida sana kwa wapenzi na washabiki wa mchezo wa ngumi kusikika wakilia kuomba usimamizi wa serikali katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Licha ya jitihada za wadau kupambana na kuhakikisha ngumi zinafikia mahali panapo vutia  lakini bado kumekuwa na matatizo kila kukicha.
Tatizo kubwa ni watu kujiendesha bila ya kuwa na usimamizi wenye mamlaka kutoka chumbo cha juu  kinachosimamia michezo nchini.
Baada ya kutokea hayo kwa takribani miaka 20, Serikali ya Rais  DR.John Magufuli imekuja na mkakati wa kuwaundia chombo cha kutengeneza sera na kanuni za kuusimamia mchezo huo wa ngumi za kulipwa nchini.
Kamati hiyo inayoundwa na watu Sita iko chini ya Mwenyekiti Habibu Kinyogoli  Katibu mkuu kwa sasa ni Chaulembo Palasa baada ya Emanuel Mlundwa kusimamishwa kufanya kazi za masumbwi nje na ndani ya nchi.
Kamati ilipata baraka za Katibu wa baraza kwenda kuandaa miongozo na kanuni za kusimamia ngumi za kulipwa nchi nzima.
Kinachostaajabisha watu hawa baada ya kupewa uhuru wa kujichaguwa wakatumia uhuru huo kujipanga wao wenyewe huku wakijuwa kati yao hakuna maelewano.
Mlundwa ambae alikuwa katibu wa kamati hiyo hana maelewano mazuri na katibu wa sasa Chaulembo Palasa mpaka kufikia kupelekana mahakamani.
Historia inaonyesha kuwa Mlundwa ndie aliyempa Chaulembo pesa na wakiri wa kusimamia  kesi iliyokuwa imefunguliwa na Onesmo Ngowi baada ya Chaulembo kuwa akimfanyia visa katika shughuli zake.
Dhumuni la kumpa pesa hiyo ilikuwa ni kumuondoa Ngowi kwenye Uwenyekiti kwa sababu kulikuwa na mwingiliano wa kimaslai kati yao.Hivyo akichukuwa Chaulembo, Mlundwa atakuwa huru kufanya biashara zake.
Cha kushangaza baada ya Chaulembo kushinda kesi uadui ukahama kutoka kwa Ngowi ukaja kwa mtu aliyemuweka yeye mwenyewe.
Kutokana na historia hiyo mvutano kati ya Mmiliki wa kampuni ya Puglistic Syndicate of Tanzania (PST) na Tanzania Professional Boxing Commition (TPBC), umeendelea kuwa kikwazo katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Baada ya mpasuko huo Serikali kwa kupitia Waziri wa Michezo Nape Nauye aliamuwa kuwaita wahusika wote wa Makampuni na Chama ili kutaka kuweka mambo sawa.
Chakushangaza ndani ya kamati hiyo iliyopewa kazi kwa miezi kadhaa tayali kunampasuko,mpasuko huo unakuja baada miongoni mwao wanaounda hiyo kamati wanamgongano wa kimaslai.
Juzi aliyekua katibu wa kamati hiyo Emanuel Mlundwa alijikuta kwenye kashfa ya kuwatumia watoto wadogo waliochini ya miaka 18, katika mchezo kati ya Thomas Mashali na Sajjad mehrab.
Nikweli watoto walitumika kinyume na taratibu maana hakuna sheria inayoruhusu watoto kuwa eneo la starehe mpaka usiku wa Saba na pia kuwatumia katika ngumi za kulipwa.
Wakati  huo tayali alikwisha andikwa na  Baraza la michezo yenye kumbukumbu namba- KVJM/MIC/SR/1/28/87 iliyokuwa ikimtaka  ajieleza kwanini asichukuliwe hatu kwa kuwachezesha utangulizi watoto Mawazo Leonard na Mbaraka Ally,  katika mechi ya Monica Mwakasanga Tanzania na Marischa Sijauw wa Uholanzi.
Hivyo kitendo cha kuwatumia watoto katika michezo Mlundwa amezoea ndio maana hakuwa na hofu kuwapandisha tena kwenye ulingo.
Kitendo cha kuwapandisha watoto kwenye ulingo kilitafasiliwa kuwa ni ukiukwaji wa haki za watoto ambazo ni kinyume cha mikataba ya umoja wa mataifa inayokataza ajira kwa watoto.
Chakushangaza Mlundwa anasema Mataifa makubwa yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa ikitolea mfano Cuba na Marekani.
Tukio hilo lilifanya vyombo vya habari kumtaka Yasin Abdallah (Ustadhi) mmiliki wa Kampuni ya Tanzania Boxing Proffesional Organisation (TPBO) kutolea ufafanuzi suala la kutumia watoto katika ngumi za kulipwa.
Ustadhi alitolea ufafanuzi kuhusiana na hilo kuwa nimakosa kuwatumia watoto kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa na ni hatalishi kwa afya zao na malezi kwa ujumla.
Lakini Mlundwa alikuja juu na kumtolea lugha chafu Yasin Abdallah (Ustadhi) kitu kilichoibuwa mtikisiko kati ya wadau wa ngumi na kupelekea wadau hao kukutana wiki moja baadae.
Mlundwa alisema sio ajabu kuwatumia watoto kwenye ngumi za kulipwa kwani mataifa makubwa yanawatumia katika huu mchezo.
Swali la kujiuliza kama Mlundwa anasema Mataifa makubwa yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa,sisi tanzania tunafuata Sheria gani ya kimataifa?
Ukichunguza kwa undani utagunduwa kuwa Mlundwa ni wakala wa kutekeleza Sheria, Kanuni na Sera za mataifa ya ulaya, ambazo hapa kwetu bado hatujaanza kuzitumia na pengine tusizitumie.
Mlundwa alienda mbali zaidi kwa kusema kama yeye amewatumia watoto na kila mtu ameona anaomba atua zichukuliwe dhidi yake lakini hao wanaomshambulia kwa kufanya vikao anaomba wasitumie kisingizio cha watoto kumziba mdomo asiseme siri zao.
Alisema wanaomchafuwa ni wale wote ambao wamekuwa na utaratibu wa kupeleka mabondia nje huku wakiwa sio mambondia na kuishia huko huko.
Mludwa alisema miezi michache iliyopita Chaulembo Palasa alitoa vibali kwa bondia watatu, na mtu mmoja ambae si bondia ambae alitambulishwa kwa hao mabondia kuwa ni Meneja wao.
Mbali na ayo Mlundwa alisema kama wao ni wasafi kwanini hawatoi maelezo ya kwanini Shomari Kimbau alirudia uwanja wa Ndege nchini Urusi, nini kilimfanya arudi ikiwa kila kitu kiliratibiwa huku Dar es salaam
Mwandishi wa makala hii hakuishia hapo aliamuwa kumtafuta Rais wa TPBC Chaulembo ili aseme huyo mtu mmoja aliyebaki Russia ni nani na kwanini Meshack Mwankemwa waliishia uwanja wa ndege Urusi alipopatikana alisema hajui hizo taarifa na anamshangaa Mlundwa kusema kunamtu kabaki Rusia.
Lakini pia suala la Kimbau na Mwankemwa kurudia uwanja wa Ndege lilitokana na Shomari kutokuwa na mawasiliano mazuri na promota wa mechi ya mwankemwa.
Embu tujiulize mtu anawezaje kutoka Tanzania mpaka Urusi bila kuwa na mawasiliano na mwenyeji wake, je hizo nyaraka walizopeleka ubalozini ili wapewe kibali cha kukaa Urusi zilikuwa hazionyeshi tarehe,mwenyeji wao na dhumuni la wao kwenda kule?
Mbali na hayo kawaida ya ngumi za kulipwa ukishakuwa na mchezo lazima utaonekana kwenye ubao wa matangazo wa kimataifa (Box rec) na ukweli mchezo wa Mwankemwa ulikuwa unasoka tarehe usika.je nini kilitokea akaishia uwanja wa ndege.
Ukiangalia kwa kina utaona kunauondokaji wa kiholela wa watanzania kwenda nje, je safari za mabondia hawa Ofisi za uhamiaji wanapata taarifa au nao huwa wanaacha watu wajiondokee hasa mabondia.
Kutokana na mlolongo huu uliojaa ubabaishaji mwandishi wa makala akapiga hodi Ofisini kwa Katibu wa baraza la MichezoAbdallah Kiganja.
Mwandishi: Ndugu Kiganja unafahamu nini kuhusiana na huu mvutano wa Kamati ya kuunda katiba ya kusimamia ngumi za kulipwa.
Kiganja: Sijapata taarifa yoyote inayohusu hii kamati iliyoundwa.
Mwandishi: Hunataarifa za Emanueli Mlundwa kutumia watoto katika mchezo wa mashali Sajjad mehrab?
Kiganja:Sina taarifa kuhusiana na ule mchezo maana sikuwepo Ofini nilikuwa safarini.
Mwandishi: Sheria za nchi kwenye masuala ya michezo inawataka watoto washiriki michezo mpaka saa ngapi?
Kiganja: Watoto mwisho saa 12,jioni,wanapaswa kuwa wamemaliza michezo yao.ikitokea wameshirikisha watoto katika michezo yao basi wazingatie taratibu zinataka nini.
Ikitokea ikadhibitika waliwatumia watoto katika mchezo ule  Baraza litachukuwa hatua kwa wale wote waliohusika katika kuwatumia hao watoto.
Kutokana na maelezo ya kiganja anapenda michezo ishirikishe watoto lakini izingatie kanuni.Je kwa  matumizi yale ya mtoto wa kike (Red Card) je ni utaratibu upi mpaka usiku wa saa Saba?
Ifikie mahali sasa Serikali ionyeshe makucha yake kwa watu wa mchezo wa ngumi maana wamejisahau wanajiendesha wanavyojisia.
Sio ajabu kusikia Gloves zikatumiwa na wachezaji wote,sio ajabu kuona watazamaji wakilaani maamuzi mabaya yanayotolewa na waamuzi wakati wa mchezo,sio ajabu kuona bondia anashuka  ulingoni hajavishwa mkanda kisha kujibiwa "Mkanda hata mbwa anao".
Kama serikali imeshindwa kudhibiti huu mchezo bora iufute ili kutoa nafasi ya kujipanga upya kuliko kuuwacha ubaki kuwa wa watu binafsi.
Huwezi kusema eti umeunda kamati ya kuandaa katiba huku walioteuliwa ndio wamiliki wa haya makapuni yaliyotufikisha hapa mbali ya kuwa wao wenyewe hawaelewani kila siku malumbano.
Tusipokuwa makini kwenye hili watamponza Waziri wa Michezo atumbuliwe kwa sababu ya njaa na uhasama wa kati ya wamiliki wa haya makampuni na chama.
hata hivyo mimi binafsi napendekeza kuwe na chombo kitakacho ratibu mchezo wa ngumi za kulipwa kwapamoja ili kusiwe na mgongano na migogolo kwa watendaji wake ila chombo kitoe ruhusa kwa mawakala wa mchezo wa ngumi kutafuta michezo mingi zaidi nje a nchi ili mabondia wapate kunufaika na mchezo wauchezao wakati wangali na nguvu zao

ni siwe mwingi wa maneno kwa leo naomba kuishia hapo ili utaratibu na maamuzi ya busara ufuate mkondo wa uongozi wa pamoja

MABONDIA WA SUPER D WAWATOA NISHAI WA MATUMLA NA MZAZI

Mabondia Vicent Mbilinyi kulia akioneshana umwamba wa kutupiaa makonde na Msafiri Haule wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbilinyi alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Vicent Mbilinyi kulia akioneshana umwamba wa kutupiaa makonde na Msafiri Haule wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbilinyi alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
WAKISUBILI MATOKEA BAADA YA KUMALIZIKA MPAMBANO

Mabondia Ibrahimu Mwaluwale kutoka kwa 'Mzazi GYM' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd Mkwela kutoka kwa 'Super D Coach' wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Idd Mkwela kutoka kwa 'Super D Coach'  kushoto akioneshana umwamba na Mabondia Ibrahimu Mwaluwale kutoka kwa 'Mzazi GYM' Mkwela alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu
Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Ibrahimu Mwaluwale kutoka kwa 'Mzazi GYM' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd Mkwela kutoka kwa 'Super D Coach' wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA IDD MKWELA KUSHOTO AKISALIMIANA NA KOCHA CRISTOPHER MZAZI BAADA YA MPAMBANO WAKE NA IBRAHIMU



Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Wawili  wanaonolewa kutoka kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 

mabondia hawo Idd Mkwela ambaye alimsambalatisha bila huruma bondia Ibrahim Mwaluwala kutoka kwa Christopher Mzazi ' MZAZI GYM'  kutoka mabibo mpambano wa raundi nne ata hivyo mpambano huu ulioanza kwa kasi ya ajabu ambano katika raundi ya kwanza

Mwaluwala alidondoshwa chini mara mbili kwa ngimi nzito nzito ilipofika raundi ya pili mabondia hawo walicheza mchezo wa piga nikupige ikafika kuangaliana kama majogoo baada ya kupigana ngumi nzito nzito katika raundi hiyo raundi ya mbili ilivyo isha ilivyo ingia raundi ya tatu Mkwela alikuja na mashambulizi mapya kabisa kwa kupiga ngumi nzito pamoja na kukwepa za mpinzani wake na mpinzani uy alivyona jahazi linazama refarii akanza kumuhesabia na kukatisha mpambano uho

na bondia mwingine Vicent Mbilinyi kutoka kwa 'Super D coach' alimsambalatisha Msafiri Haule kutoka katika clab ya mchezo wa masumbwi ya 'Matumla' inayo ngozwa na bondia mkongwe katika masumbwi Rashid Matumla mpambanowa raundi Sita

na Mbilinyi kuibuka na ushindi wa point ushindi huo uliopokelewa kwa furaha na kocha wa mchezo uho 'Super D' ambapo amesema uhu ni mwanzo tu wa mabondia wake kukutana na nguli wa mchezo wa masumbwi na hizi ni kama salamu kwa mabondia wengine wakitaji kucheza na mabondia wangu wajipange sana vinginevyo watakumbana na kipigo kibaya sana ambacho awataweza kusahau


BONDIA IDD MKWELA AMPIGA K,O YA RAUNDI YA TATU IBRAHIMU MWELUWALA WA MZAZI GYM











BONDIA VICENT MBILINYI ALIVYO MGALAGAZ MSAFIRI HAULE

Mabondia Vicent Mbilinyi kulia akioneshana umwamba wa kutupiaa makonde na Msafiri Haule wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbilinyi alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kulia akioneshana umwamba wa kutupiaa makonde na Msafiri Haule wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbilinyi alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Vicent Mbilinyi kulia akioneshana umwamba wa kutupiaa makonde na Msafiri Haule wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbilinyi alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Msafiri Haule kushoto akineshaa umwamba na Vicent Mbilinyi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndandi wa taifa mbilinyia alishinda kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Msafiri Haule kushoto akineshaa umwamba na Vicent Mbilinyi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndandi wa taifa mbilinyia alishinda kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
MABONDIA VICENT MBILINYI KUSHOTO NA MSAFIRI HAULE WAKISUBILI MATOKEO KATIKA MPAMBANO WAO ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA

MATOKEO BAADA YA KUTANGAZWA

Friday, June 3, 2016

MABONDIA VICENT MBILINYI TOKA KWA SUPER D NA MSAFIRI HAULE TOKA KWA MATUMLA KUPAMBANA JUNI 4 TAIFA

BONDIA VICENT MBILNYI  KUTOKA KWA'SUPER D' KUSHOTO AKITAMBIANA NA MSAFIRI HAULE KUTOKA KWA 'MATUMLA' GYM BAADA YA KUPIMA UZITO KWA AJILI YA KUZIPIGA JUNI 4 UWANJA W NDANI WA TAIFA

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA wawili kutoka katika GYM mbili tofauti zenye uhasimu wa kutaka kujua nani zaidi katika clab hizo zinazo ongozwa na mabondia wa siku nyingi

utakao usisha Bondia Vicent Mbilinyi anaefundishwa na kocha wa kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' na Msafiri Haule anaenolewa na bondia mkogwe katika mchezo wa Masumbwi Rashidi Matumla anaetokea katika familia yenye vipaji lukuki vya mchezo wa masumbwi nchini 

Mabondia hawo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi sita katika uzito wa kg 63

mpambano uho wenye lengo la kuwainuwa mabondia na kupata viwango vya kueleweka katika mtandao wa boxing nchini
mpambao uho utakaofanyika juni 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa 

katika mpambano uho kutakuwa na apambano mengine ya kusisimua ambapo bondia Cosmas Cheka atagombania mkanda wa ubingwa wa U.B.O pambano la raundi 12 na Chrispin Moliyati wa Malawi

mpambano mwengine utawakutanisha mabondia Yonas Segu na Wilson Masamba kutoka Malawi

mipambano mingine ya kimataifa yaa wakutanisha mabondia wa kike Lulu Kayage wa Tanzania atakaezipiga na Will Eneles kutoka Malawi
wengine ni Japhert Kaseba atazidunda na Amour Mzungu kutoka Zanzibar na Ashiraf Selemani kutoka Zanziba atakumbana na Elick Gogodo wa Malawi katika mchezo wa uzito wa juu kabisa
wakati Alphonce Mchumiatumbo atakabiliana na Mussa Ajibu kutoka Malawi mpambano wa raundi sita
siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi pia ngumi zitaanza mapema kuepusha usumbufu unaojitokezaga kwa wapenzi kuchelewa majumbani mwao kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba sheria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo

Maskini Muhammad Ali! Alazwa tena hospitalini


https://i.ytimg.com/vi/C_fEIVwjrew/maxresdefault.jpg
Muhammad Ali katika moja ya mapambano yake akimuadhibu mpinzani wake aliyelala sakafuni.
UNAMKUMBUKA Bingwa wa Dunia wa Masumbwi uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali? Ni hivi. Jamaa huyo aliyewatetemesha mabondia wenzake amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu.
Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa katika hali wastani alipolazwa hospitalini.
Hata hivyo familia yake ilipendekeza alazwe hospitali kama tahadhari kwa sababu mbali na maambukizi hayo Ali anaugua kiharusi.
Bondia huyo alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu mchezo huo wa ngumi za kulipwa.
Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita baada ya kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.
Chanzo: BBC Swahili

NGUMI ZA KIMATAIFA KUPIGWA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA JUNI 4

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota wa mkanda wa ubingwa wa Dunia wa U.B.O Juma Ndamile kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mpambano uho pamoja na upimaji uzito kwa mabondia wengine ni Kulwa Makaranga na bondia Cosmas Cheka atakaegombania ubingwa wa Dunia na Chrispin Moliyati mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Lulu Kayage kushoto akitunishiana misuli na mpinzani wake Will Enelesi wa Malawi mpambano wao utafanyika juni 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ashiraf Selemani kutoka Zanzibar  kushoto akitunishiana misuli na ElickGogodo wa Malawi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Cosmas chka anapanda uringoni kugombania ubingwa wa Dunia wa U.B.O kwa kupambana na Chrispin Moliyati kutoka Malawi mpambano wa raundi 12

wakisindikiza na mabondia chipkizi ambapo bondia kutoka katika kambi ya 'Super D' Vicent Mbilinyi ata kabiliana na bondia kutoka kambi ya akina ukoo wa Matumla Msafili Haule watazipiga katika uzito wa kg 63 mpambano wa raundi 6

mipambano mingine ya kimataifa yaa wakutanisha mabondia wa kike Lulu Kayage wa Tanzania atakaezipiga na Will Eneles kutoka Malawi

wengine ni Japhert Kaseba atazidunda na Amour Mzungu kutoka Zanzibar na Ashiraf Selemani kutoka Zanziba atakumbana na Elick Gogodo wa Malawi katika mchezo wa uzito wa juu kabisa

wakati Alphonce Mchumiatumbo atakabiliana na Mussa Ajibu kutoka Malawi mpambano wa raundi sita

siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi pia ngumi zitaanza mapema kuepusha usumbufu unaojitokezaga kwa wapenzi kuchelewa majumbani mwao kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba sheria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo
 

Wednesday, June 1, 2016

TASWA YAUNDA KAMATI YA TUZO ZA WANAMCHEZO BORA TANZANIA 2015/2016


DAR ES SALAAM
 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko (pichani), kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
 
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza (Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
 
Kamati inaweza kuongeza wajumbe wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
 
Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
 
TASWA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine la waandishi wa habari chipukizi.
 
Kwa kuanzia wahariri wa habari za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
 
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
 
Imetolewa na :
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016